
Kama umeamua kula kondooo kula aliyenona haswaaa, Kiasi kwamba hutojutia kabisa hata kama alikuwa kondoo wa wizi
Ukiamua kutenda dhambi basi itende haswaaa maana hakuna dhambi ndogo
Mfano umeamua kuiba sasa kwanini unaiba kitu kidogo? Ikitokea umekamatwa yani upo tayar kuuliwa kisa kitu chenye thamani ndogo?? Kweli!?
Ukitaka kuwa mtakatifu basi jitakase haswaaa maana dini haina majaribu wala haitaki utani
Ukiamua kufanya Biashara ifanye haswaaa kwa uwezo wako wote kiasi kwamba hata kama ukishindwa usibaki na dukuduku na ukishinda usemee eeh yes kwa nguvu kubwa…
Kamwe kamwe usiwe mtu kati katika maisha yako
Kwamba hukai wala husimami, huendi wala haurudi kiufupi upo kama hujui nini unataka!
Simama eneo moja ujulikane na vaa uhusika uliouchagua wote hata kama unafanya jambo dogo zuri au baya
Fanya mpaka wengine wameze mate na watamani kuiga mfano wako hata kama nyuma walikupinga.
Jiamini na amini kwenye njia uliyoichagua kwa asilimia zote hata kama ni njia ndogo.