
Changamoto za leo kuna siku utazisahau hata historia yake
Magumu ya sasa kuna muda utashindwa hata namna ya kuyaelezea kama yalivyokuwa
Shida za leo kuna wakati hutokumbuka chochote kilichokutokea
Kilio cha sasa itafika muda utajiuliza kwanini ulikuwa unalia
Uchungu uliokujaa leo moyoni kuna siku utajilaumu kwanini ulipatwa na simanzi kama hio
Ijue thamani yako, simama imara, kaza roho na zikabili changamoto zako kupitia imani yako…
Jipe muda, muda ni mwalimu mzuri sana hakika muda utakupa unachotaka
Usikubali kuumia kwa sababu zingine zozote hapa Duniani hata kama zina ukweli wowote
Maisha ni zawadi ya muda mfupi sana, jifunze kufurahia kila sekunde uliyonayo sasa.