
Siku utakapojua kuwa watu wanaosema wanakupenda kwa sasa kuna siku watawaambia maneno hayahayo watu wengine Ndio siku utayojua kuwa unapaswa kuiamini nafsi yako pekee!
Siku utakayoelewa kuwa ikitokea umekufa waliokaribu yako wote watakusahau ndani ya muda mfupi na kuendelea na maisha yao Ndio siku utaacha kuishi kwa kutaka kumridhisha kila mtu
Endapo utaelewa kuwa kila anaeonesha kama anakufatilia na kukuchunguza kiuhalisia wala hana muda na wewe na anaumizwa na maisha yake binafsi Ndio ungegutuka na kuishi maisha yako bila kuogopa watu
Kama ungepata nafasi ya kuoneshwa siku utakayokufa basi uhakika ni kuwa kuna mambo mengi usingeyafanya hapa Duniani hasa kuumia kwa ajili ya vitu vinavyopita.
Maisha ni yako na wewe ndio dereva hivyo yaendeshe upendavyo.