Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Tafuta Upekee Wako

tafuta upekee wako
Photo by Markus Spiske on Pexels.com

Usikubali kuwa wa kawaida wala kufanya mambo wanayofanya wengine na yaliyozoeleka

Mafanikio huja kwa kufanya vitu hata kama ni vidogo vidogo lakini katika njia ya kipekee

Tafuta ladha yako mwenyewe usiige watu wengine

Fanya kwa namna yako ambayo italeta msisimko katika milango ya fahamu ya wateja na mashabiki zako

Wafanye wateja wapate hisia tofauti, ladha ya kipekee na hata waone vitu ambavyo hawaja zoea kuviona kwenye macho yao

Watu waliofanikiwa zaidi sio kwamba ni watu maalumu sana au wenye nyota sana wala wana kibali cha peke yao

Bali walifanya mambo yao katika namna ya tofauti na kipekee bila uoga (ubunifu wa ziada)

Epuka kuwa wakawaida, kama unafanya mambo sahihi na unajua nini unafanya basi USIOGOPE KUONEKANA TOFAUTI.

Anza sasa kujiuliza kwenye hicho hicho kidogo unachokifanya unawezaje kujitofautisha na wengine?

USIKUBALI KUFANANA NA WENGINE UMEUMBWA KUWA WA KIPEKEE.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Tengeneza Bahati Yako Mwenyewe

Next Post

Chagua Changamoto Zako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Tengeneza Mabawa Yako

Usikubali mazingira yakwamishe ndoto zako wala kukupa vikwazo vya kuwa unavyojiona kwa ndani Usikubali watu…

Usiogope Kujaribu

Usiogope kujaribu jambo hata kama unahisi huliwezi au ni gumu sana Kataa kabisa neno haiwezekani kwenye akili…

Kula Kondoo Aliyenona

Kama umeamua kula kondooo kula aliyenona haswaaa, Kiasi kwamba hutojutia kabisa hata kama alikuwa kondoo wa wizi…