
Ukipata nafasi ya kusaidia mtu unapoweza msaidie kwa moyo mmoja..
Ukipata nafasi ya kuonesha uwezo hakikisha unaonesha uwezo wote bila kuogopa
Ukipata nafasi ya kufurahi hata kama ni muda mchache jitahidi kutumia muda huo kufurahia kama vile hutofurahi tena!
Ukiona nafasi ya kufanya jambo hata kama ni dogo basi lifanye kwa ubunifu wako wote,
Ukiwa na nafasi yakuwa na familia yako, ndugu jamaa na marafiki basi itumie kwa ukamilifu wake wote
Fanya hivyo kwasababu maisha hayatupi nafasi zaidi, kuna uwezekano mkubwa nafasi uliyopata leo usiipate tena kesho
Hatujui kesho yetu wala hatuna uhakika wa sekunde ijayo..
Lolote linaweza kutokea wakati wowote hivyo tunapaswa kuishi kwa tahadhari na kuyachukulia mambo katika upande Chanya bila kubeba maumivu wala kusababisha maumivu kwa wengine.