
Kauli hii ni miongoni kati ya Kauli ambazo tumezizoea kwenye maisha yetu
Ukweli ni kuwa imebeba maana kubwa ya utafutaji ambayo wengi hawaijui
Pia asilimia kubwa huichukulia Kauli hii kwa namna ya wepesi sana bila uzingativu kabisa
Sasa tukirudi kwenye maisha na harakati za kutafuta mkate wa kila siku..
Maana yake ni kuwa siku zote anaetoka kutafuta hata kama hajui anapoenda au atapataje anachotaka..
Hawezi kuwa sawa hata kidogo na yule aliye amua kulala au kukaa ndani kisa hana pakwenda wala hana sababu ya kutoka
Kuzunguka mtaani au ambapo unahisi unaweza kupata Rizki… au hata Kutokuwa na sababu yoyote
Hakika sio sawa na yule aliyejifungia ndani kabisa
Kwenda sehemu yoyote hata kama hupajui bado sio sawa na kukaa ndani
Usikubali kujifungia ndani eti kisa huna pakwenda wakati huo huo huna uhakika wa kipato
Toka nenda hata mtaa wa pili, nenda vijiweni, nenda masokini, nenda hata sehemu za sterehe za bure kama fukwe za bahari….
Nenda popote pale kwenye mkusanyiko wa watu mbali mbali hakika hutobaki kama ulivyoenda
Jifunze wanachofanya, ongea na mtu yoyote hata kama humjui kabisa hakika utapata mwanga na utajifunza jambo linaloweza kukusaidia
Usikae ndani wakati huingizi chochote, usijifunge ikiwa huna uhakika wa kula wala kipato cha maana
Toka kazunguke, ongea na watu wageni machoni kwako, Jichanganye na ukiweza chukua mawasiliano yao
Ukiwa mtu wa kutoka hata kama huna sababu hakika ndani ya mwezi mmoja tu utajua uanzie wapi kujikwamua.
Lakini pia unapotoka hata Mungu huweza kukukutanisha na muujiza wako njiani tofauti na kujifungia ndani huku unaomba maombi!
Bahati haitengenezwi chumbani kwako bali bahati inapatikana nje kwenye mzunguko wa watu wengi.
KUMBUKA PENYE WENGI KUNA MENGI.