Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Kuna Wakati Amani Ni Bora Kuliko Ushindi

Sio lazima utumie nguvu kubwa sana kutaka kuonekana mshindi!

Kuna muda ukimya wako tu unatosha kummaliza adui yako

Sio kila jambo linataka majibizano wala mapigano ya nguvu..

Sio kila kitu lazima kikuchukulie muda wako

Kuna vitu vinapaswa kuachwa kama vilivyo

Kuna washindani wanapaswa kuachwa kama walivyo

Kama jambo halimalizi afya yako wala haligusi moja kwa moja kipato chako Acha lipite!

Kuna wakati unaweza kujikuta unapambana na mtu ambae furaha yake ipo kwenye ugomvi

Kuna muda utajikuta unaumizwa na mtu ambae furaha yake kukuona unaumia

Usikubali kumpa mtu mwingine furaha wakati huo huo unaumia wewe mwenyewe

Acha lipite kwa ajili ya amani ya moyo wako

Ukiwa na amani huwezi kukosa kitu chochote hapa Duniani

Amani Ndio daraja la afya bora na afya Ndio msingi wa mafanikio!

Jifunze kukaa kimya na kuacha mambo madogo madogo yapite kama yalivyo

Ukimya wako ni silaha kubwa kwa adui ambae amejipanga kugombana na wewe

Adui aliyejipanga kukuharibu kiakili mjibu kwa ukimya wako

Mshindani aliyejipanga kukuchafua jina, mjibu kwa ukimya wako

Acha asili iamue, Acha maji yafuate mkondo wake

Kama una uhakika unafanya jambo sahihi bila kuwa chanzo cha changamoto mlizonazo basi chagua upande wa amani yako kuliko ushindi wake.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Mtembea Bure Si Sawa Na Mkaa Bure

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next