
Jitahidi sana furaha na amani yako vikutegemee wewe mwenyewe
Usikubali kabisa furaha yako iwe kwa mtu mwingine wala kitu kingine
Yani unapaswa kuwa chanzo cha furaha yako bila utegemezi mwingine wowote
Bila kujali mazingira uliyopo kwa sasa au kwa baadae
Bila kujali watu wanao kuzunguka sasa au hata baadae
Na bila kujali vitu unavyo miliki sasa au hata baadae
Kwa maana kwamba hata kama kitu, watu au mazingira vikibadilika basi wewe unapaswa kubaki vile vile
Ikitokea umesalitiwa na kuachwa na mtu yoyote unapaswa kubaki vile vile
Endapo utabadili mazingira yako kwa namna yoyote ile unapaswa kuwa na furaha ile ile
Na ikiwa utapoteza kitu chochote hata kama ni kitu cha thamani sana unapaswa pia ubaki na furaha ile ile
Yaani hupaswi kabisa kuishi kwa ajili ya kitu, mazingira au mtu
Elewa kuwa watu wana badilika muda wowote na vitu vinaweza kupotea wakati wowote pia mazingira hubadilika wakati wowote!
Usiwe mtu ambae utapoteza muelekeo wako kisa watu wengine, mazingira au vitu vingine
Furaha yako inapaswa kutoka ndani yako wewe mwenyewe
Ndani ya moyo na roho yako bila kusahau mwili wako
Jipende kiasi kwamba huhitaji mtu mwingine kukusaidia upendo ili kujiona umekamilika
Jipende kwa kiwango kuwa hata kama utapoteza kila kitu na kuanza upya kabisa bado hutoweza kujipoteza wewe mwenyewe
Jipe furaha kwa kadiri unavyoweza hata kama itagharimu kila ulichonacho
Ila kamwe usipoteze chochote kwa ajili ya mtu mwingine kukutunzia furaha yako.