
Kwenye maisha kila mmoja yupo katika nyakati zake na muda wake sahihi
Usijione umechelewa sana ukahisi Mungu amekusahau
Usikose raha kisa mafanikio ya mtu mwingine aliyekutangulia
Kumbuka kutangulia sio kufika wala kuchelewa sio kukosa!
Maisha yana mzunguko wake kwa kila mtu, hakuna bingwa sana wala mjinga sana
Unaweza kuchelewa kupata lakini ukapata kilicho bora zaidi
Au hata ukadumu nacho miaka mingi zaidi,
Mwingine anaweza kutangulia kupata na akakipoteza ndani ya muda fulani au akapata kisicho bora kama chako
Kuna watu wametangulia kuoa au kuolewa Ila wakaachika
Kuna watu walipata kazi mapema na wakafukuzwa au kupoteza nafasi zao
Kuna ambao waliotangulia kupata watoto lakini wakawapoteza au hata kuteseka na uzao wao
Kuna wale waliowahi kupata pesa na wakafirisika!
Usisahau kuna ambao walikuwa watu wa dini sana na wakaishia kutenda maovu
Hivyo usiyaonee tamaa mafanikio ya mtu mwingine kabisa
Usijione upo mbali sana na wale walio mbele yako
Kama unafanya jitihada kila siku za kusogea unapotaka basi usiumizwe na muda wala usijilinganishe kama wengine
Fanya jitihada zako kwa kujilinganisha na ulipotoka yaani jana yako
Muombe Mungu akusaidie na akuzidishie kiwango cha imani bila kusahau subra
Najua kuna muda unapitia nyakati za kukata tamaa
Sio rahisi kuona wengine wapo mbele na wewe nyuma kila siku
Inaumiza sana na hata kukufanya uone kama maisha si kwa ajili yako
Lakini subiri wakati wako hakika utasahau maumivu yote unayopitia na utashangaa hata kwanini ulitamani maisha ya wengine.
Mwajuma Muhasu
Lifewithmuhasu.com