
Kuna watu wengi sana walikariri ule msemo wa samaki mmoja akioza basi wote wameoza
Hii imefanya watu kupoteza mambo ya muhimu sana kwenye maisha yao
Kwa kulinganisha msemo huo wa wazee kwenye maisha halisi!
Si kila msemo unafaa kutumika kwenye maisha ya kila siku
Mfano huwezi kusema wanaume wote wanafanana tabia kisa mwanaume mmoja au wengi walio kuumiza
Au wanawake wote wapo vile vile kwa matendo yao kisa mwanamke alokutenda
Na hata marafiki wote ndivyo walivyo wapo kimaslahi tu na wanafiki, kumbuka sio marafiki wote wapo hivyo
Au tuseme kundi la watu fulani wote wahesabike kwa makosa ya mwenzao mmoja! Labda kundi la marafiki wa mwizi fulani
Ukiona jambo moja limeharibika toa weka pembeni endelea na mengine
Lakini hata samaki yule yule aliyeoza anaweza kuwekwa viungo na akabaki na utamu ule ule wa mwazo!
Inategemea na utundu wa mapishi tu!
Kwa maana kuwa mtu au kitu kinaweza kuharibika na kikatengenezwa upya! na hata watu hurekebishika
Sio kila jambo linapaswa kuhukumiwa kama lilivyo au kwa makosa ya watu wengine
Kuna vitu vipo kwenye mazingira yasiyo faa kabisa lakini havina uhalisia wa mazingira vilivyopo
Jifunze kutumia busara na akili kwenye kuchanganua mambo na hata kufanya maamuzi sahihi
Bila kulinganisha mambo ya kusadikika na uhalisia uliopo
Yaani usiishi kwa mazoea na kukariri mambo yale yale kila siku
Kuna wakati utapoteza vitu au watu wa msingi kwa sababu za kukariri tu.