
Hizo changamoto zote unazopitia wala usihesabu kama mateso
Shida na mitihani uliyo nayo wala usichukulie kama kuteseka
Mazito na mapito yanayo kuandama wala usijione kama una teseka
Elewa kuwa hayo yote yanakupa ukomavu wa akili na mwili wako
Uzoefu wa hayo unayo pitia leo kuna siku utasema ningejua ningepitia mengi zaidi
Ipo siku utajipongeza kwa maisha ya sasa au zamani uliyo pitia
Kuna muda utafika utasahau hata maumivu yalifafanaje
Lakini utabaki na mafunzo ambayo kamwe hayato kuyumbisha kabisa tena
Hata dhahabu ili inga’e hupitishwa kwenye moto mkali sana
Hivyo jione kama dhahabu ya baadae
Jione mshindi wa baadae na hata jasiri wa baadae
Ujasiri unao jengewa kwa sasa huwezi kuuelewa mpaka muda ukifika
Kama unaona kupata hasara ya laki moja ni sawa na kupoteza kila kitu! Utaweza kuvumilia maumivu ya kupoteza milioni 10?
Kama unapata maumivu yasiyo isha kisa kuachwa na mwanaume kwa sasa ukiwa huna hata mtoto! Utaweza maumivu ya kuachwa na watoto 3?
Ikiwa unaumia kukosa kazi kwa sasa na huna familia! Utaweza kuhimili heka heka za kukosa kazi ukiwa na familia inayo kutegemea!?
Kumbuka yote ya sasa yanakuandaa kwa wakati ujao ambao unaweza kupitia au usipitie kabisa
Jambo la msingi ni kuwa imara kama vitani, hata kama hujui muda wa kuvamiwa lazima uwe na silaha zote!
Ujasiri wa maisha unafundishwa kupitia mchakato wa uzoefu wa changamoto za kila siku
Zipokee changamoto zako na zitatue wewe mwenyewe kwa niaba ya kesho yako.