
Jifunze kupokea mabadiliko ya watu wengine
Watu hukosea, hujifunza na huanza upya na kutamani kusahau kila kitu cha nyuma
Usiwe mwepesi sana wa kuishi kwa kukariri maisha ya zamani
Mtu anapo onesha kujuta na kubadilika, mpe ushirikiano
Watu wengi sana wamewahi kufanya mambo mabaya sana lakini kuna muda hufika na kuamua kubadilika
Hakuna ambae hakosei au hajawahi kosea kwenye maisha yake iwe zamani au baadae
Kila mtu ana historia fulani mbaya ndani yake yaweza kuwa ya siri au dhahiri kwa wengine
Kukosea sio tatizo wala sio sababu ya kumpa mtu alama na kilema cha maisha
Maisha yana badilika sana, mambo mengi hutokea na kufanya watu kuanza upya
Usiwe mtu unaependa sana kushadadia maisha ya wengine hasa yale ya zamani
Pokea mabadiliko ya watu kwa namna ambavyo wanaonesha jitihada za mabadiliko
Wape watu ushirikiano ambao hata wewe utatamani kupata endapo utataka kuanza upya
Hatupaswi kuhukumu makosa ya watu hususani kama wamejua walipokosea
Maumivu ya kumbukumbu mbaya za zamani yanatesa sana hasa pale unapoona wengine wanakufanya ukumbuke kwa lazima
Acha maisha mengine yaendelee kwa watu wanapotaka kujitafuta upya na kurekebisha historia zao.