
Watu wote wanao kuzunguka kuna siku watakuacha!
Wale wanao onesha kukupenda sasa, kuna siku watakuacha!
Wale wote unao ona mnakula bata na good times sasa, ipo siku hutowaona kabisa
Hao ambao wanakuambia maneno mazuri muda huu, kuna siku hutopata hata salamu zao!
Maisha huleta na kuondoa watu kila wakati
Kama hujihisi kukamilika bila kuzungukwa na watu basi wewe ndio tatizo lenyewe!
Haijalishi una sababu za msingi kiasi gani, jifunze kuishi na kujitegemea mwenyewe
Wakati wa shida na wakati wa raha, zoea kuwa mwenyewe
Jipe furaha muda wa mazuri na jipe kumbatio la faraja wakati wa shida
Ukiwa na mazoea ya kuwa mkamilifu bila kuwa na wapambe pembeni maisha yatakuwa marahisi sana kwa upande wako siku zote
Elewa kuwa ulizaliwa mwenyewe na utazikwa mwenyewe
Yaani Mungu mwenyewe anajua kuwa kila mmoja anaweza kuwa peke yake na hakuna tatizo katika hilo
Changamoto huja pale unapotaka kukumbatia kila mtu wakati wote
Sio vibaya kuwa na watu Ila ubaya huanzia pale unapotaka wabaki upande wako nyakati zote!
Jifunze kuwa mwanajeshi na jeshi la mtu mmoja, peke yako unatosha kukamilika
Huhitaji mwingine wa karibu kukufanya ucheke, ulie wala ustarehe.
Watu wamejaa kila mahala utakapo enda, ukihitaji kampani za muda zipo kila sehemu
Sio lazima kuwa na watu kwapani ambao wanajua undani wako na kila unachopitia ndio ujione kama umetimia!
Nenda popote na furahia maisha yako mwenyewe, wakija acha waje na wakiondoka acha waende
Kitu cha msingi ni kuwa iwe wapo au hawapo bado hakuna kitakacho pungua kwako.