Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Binaadamu Husahau Mema Haraka, Usijimalize Sana

Binaadamu hawana shukurani wala kumbukumbu kwenye mema na mazuri , usijimalize sana

Katika viumbe hai ambayo hupoteza uwezo wa kukumbuka mema haraka ni binaadamu

Binaadamu hata umpe roho yako, kuna siku atasahau kila kitu

Hakuna binaadamu mwenye uwezo wa kutunza mema milele

Wala hakuna binaadamu ambae hukumbuka mema aliyotendewa kwa namna ya uzito ule ule

Kosa moja tu hufuta kumbukumbu zote nzuri ulizompa

Ukitaka kukumbukwa milele tenda mabaya na maovu Ila kama unataka kusaidia pekee bila kukumbukwa basi tenda mema kisha nenda zako

Watu ni wepesi wa kukumbuka mabaya haraka mno na wazito wa kukumbuka mema

Hivyo kama unatoa kitu iwe kikubwa au kidogo kwa lengo la kulipwa mazuri zaidi mbeleni ndugu yangu unapoteza nguvu zako

Toa kwa nia njema kisha sahau kabisa, kama utakumbukwa sawa na kama ukisahaulika pia sawa

Ila tambua binaadamu yoyote uwezo wa kukumbuka mazuri ni mdogo sanaaaaa

Tenda mema 2000 kisha kosea 1 tu vidole vyote vitakugeukia

Mpe mazuri 100 sahau 1 tu basi mazuri yote yatafutwa haraka

Lakini pia akipata anapopewa zaidi ya unavyompa hapo ndio msaada wako hugeuka kama debe moja la maji baharini

Hivyo Basi usijamalize sana kisa watu haijalishi uhusiano wako na wao

Usijisahau kujipa furaha na kutumia vyako kisa shida za watu

Usiweke roho yako rehani kisa kusaidia sana watu

Na ikitokea umesaidia fanya kama umeangusha au umepoteza tu

Kamwe usitunze kumbukumbu na kutaka kulipwa sawa na ulichotoa.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kubali Uhalisia Kuna Mambo Hayabadilishiki

Next Post

Mungu Hakuumba Binaadamu Kwa Uwezo Mkubwa Awe Mzururaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.