
Kama unataka kulipa kisasi kizuri sana chenye akili kubwa na kinachouma zaidi
Basi kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa awali!
Hakuna kisasi kizuri ambacho huumiza mtesi au adui yako kama kukuona umefanikiwa zaidi ya mwazo
Hakuna kisasi kitamu ambacho humnyima usingizi adui yako kama kukuona umepiga hatua zaidi
Achana na mambo ya kurogana au kuumizana maana kuna uwezekano mkubwa ukaumia wewe zaidi
Usipoteze muda, nguvu na pesa zako kumuumiza adui yako yoyote
Kwasababu utajiumiza wewe mwenyewe na pengine kumpa yeye sababu au furaha zaidi
Adui yoyote lengo lake kubwa ni kuona unateseka au unaharibikiwa zaidi
Sasa akiona mambo yameenda tofauti, humfanya akose raha na kujiona mjinga
Hivyo basi huna sababu za kugombana na mtu wala kurushiana maneno
Ikibidi usitake hata kujua atafanya nini baada ya yote hayo kiufupi msahau na mpuuze kwa muda
Weka pamba sikioni kabisa, ikibidi vaa mawani meusi na jifanye huoni kitu
Na hata badilisha kila unachoweza na kisha wekeza nguvu, pesa na maarifa yote kuwa bora kuliko awali
Badili matazamo wako wote, hamisha nguvu zako zote na weka akili yako kwenye mambo yanayo kujenga zaidi
Hamishia hasira zako zote kwenye maisha na malengo yako muhimu
Gombana na ndoto zako kwanza kabla hujagombana na yoyote
Lilia malengo yako kwanza kabla hujatoa chozi kisa adui na mtesi wako
Weka visasi kwenye malengo yako binafsi yaliyo kwama kwanza kabla hujataka kulipa kisasi kwa adui yako
Tukana malengo yako ambayo hayaja fanikiwa kwanza kabla hujatukanana na adui yako
Kiufupi adui yako wa kwanza yawe malengo na ndoto zako
Yashinde malengo yako kisha adui wa pembeni utakuwa umemshinda kuliko unavyodhani
Utamuua adui yako halisi akiona mafanikio yako kwa mbali huku yeye akiwa amebaki vile vile
Hakuna kitu kinauma kama mtu akujibu kwa vitendo vya mafanikio zaidi.
Kwahio kuanzia sasa usigombane na mtu ugomvi usio na mashiko
Gombana na maisha yako kisha adui yako atajimaliza yeye mwenyewe kupitia maumivu ya mafanikio yako.