
Haipendezi kila wakati kulilia shida zako kwa watu
Sio busara kila saa kutangaza matatizo unayopitia
Wala sio kitu chema sana kuzungumza changamoto zako kwa kila mtu
Elewa kuwa kila mmoja ana shida zake binafsi
Kulia lia shida kila saa hukera watu, unajidhalilisha binafsi na unaondoa uhusiano mzuri baina yako na wengine
Hakuna ambae hana uhitaji wa kitu fulani au msaada fulani
Ila huamua kufa na TAI shingoni mwao kwakua huelewa hata wengine wana shida zao pia
Kuna mtu ukikuta analalamika kuwa hajasaidiwa na ndugu au rafiki zake,
Unaweza hisi aliwekeza huo msaada kwao hao watu kwa lengo la kurudishiwa siku atakapo hitaji!
Yani mtu mwingine ni mkubwa sana kiumri, Ila ukisikiliza maongezi yake utachoka kabisa
Kila saa ni shida hii, mara shida ile, mara malalamiko Haya mara malalamiko yale
Hana muda wa kuongea mambo mazuri yanayo leta furaha
Hana muda wa kusambaza nguvu chanya kwa wanao mzunguka
Zaidi ya malalamiko na vilio vya shida, hakuna kipya unaweza jifunza kutoka kwake!
Hali ya kupenda kusaidiwa kila wakati ndio hufanya akili kukosa uchanganuzi wa matatizo
Ndio imefanya wadada kudanga na wakaka kubadili utu wao
Hufanya akili kulala usingizi mzito na kutowaza chochote
Zaidi ya msaada na kitonga au mterezo kutoka kwa wengine kama ganda la ndizi,
Hupelekea tatizo linapotokea tu, akili hukimbilia kutafuta mtu wa kusaidia!
Na hii ndio imefanya hata viongozi wetu wakubwa wa nchi kutwa kutembeza mabakuli ya kuomba msaada
Licha ya wingi wa Rasilimali zilizopo, akili zao zinashindwa kabisa kuchanganua namna ya kuleta maendeleo kwa kutumia utajiri wa asili tulionao
Ila haraka hupata mbinu na mikakati ya kuomba misaada na mikopo nchi za wengine
Taifa haliwezi kujikwamua kupitia misaada haijalishi msaada wa mtu mmoja mmoja au nchi nzima
Tunapaswa kutumia akili zetu kuleta mapinduzi kwanza maeneo mbalimbali
Kisha msaada huombwa pale ambapo inalazimika Kuombwa na sio kwenye kila kitu
Hakuna jambo baya kama kujiona muhitaji wa kusaidiwa kuliko wengine
Kujiona dhaifu na kutaka kuonewa huruma kutoka kwa wengine
Hakika hii ni moja kati ya vitu ambayo mimi binafsi huninyima usingizi
Na hata kukosa hamu ya kula kabisa napokutana na mtu mzima anaomba msaada au analalamika eti hasaidiwi!
Badilisha namna unavyo fikiria, ongeza uwezo wa kutatua matatizo yako bila kuhitaji msaada wa wengine.
KUFA NA TAI SHINGONI KWENYE BAADHI YA SHIDA ZAKO