
Maisha sio sehemu ya kushindana kati ya mtu na mtu mwingine kwenye mafanikio aina yoyote
Haijalishi unataka mafanikio kwa kiwango gani, kamwe hupaswi kushindana na mtu
Kama unataka mashindano basi shindana na jana yako
Shindanisha mwaka wako huu na mwaka wako uliopita
Shindanisha mwezi wako huu na mwezi wako uliopita
Lakini pia shindanisha mafanikio uliyonayo sasa na mafanikio yako yaliyopita
Kamwe huwezi kuwa na furaha ya dhati kama utataka kumshinda kila mtu kwa sababu kadiri utakavyo pambana kuwa juu, kuna mwingine pia atataka kuwa juu yako zaidi
Hivyo utapoteza muda mwingi kutaka tena kuwa juu ya yule na pengine usiweze kabisa, muda ambao ungetumia kufurahia maisha yako!
Jambo la msingi zaidi unapaswa kuwa bora kuliko ulivyokuwa awali
Kama una maisha yanayokupa furaha, una vitu muhimu na bado unapambana kuwa bora zaidi, basi inatosha.
Hupaswi kuwa mvivu wala hupaswi kushindana na mtu yoyote yule
Kwani watu wana siri nyingi mno kwenye mioyo yao na wala huwezi jua wanayo pitia!
Pengine mtu unaekesha kutaka kushindana nae, na yeye kwa siri anakesha kutaka kukukomoa!
Au yule unaehisi ni bora na amejipata sana, kumbe nyuma ya pazia anapitia magumu na mazito mengi
Pia usisahu kuna wale ambao kwa nje unaona wamefanikiwa mno Ila kwa ndani yao wanatamani kuwa na maisha kama yako!
Ndugu yangu kamwe kamwe kamwe usiwe mtumwa wa mafanikio ya wengine
Usiumie kisa maisha na mafanikio ya mwingine haijalishi anaonekanaje kwa nje
Komaa na pambana kuboresha maisha yako wewe mwenyewe kwa njia zako
Angalia jana yako kisha utajua kama umefanikiwa au umerudi nyuma
Kumbuka kuna uwezekano mkubwa una maisha mazuri sana kuliko hao wengine unao watazama kwa nje.