
Usikubali kabisa tamaa na mapito ya maisha, zikufanye ubaki na kilema cha kudumu
Kuna mambo hayabadiliki hata kama yatasahaulika kwa muda
Kuna mambo hayafutiki hata kama utatumia ufutio wa gharama kubwa sana kufuta
Na kuna vitu alama zake hutengeneza kumbukumbu za milele tena za kudumu!
Leo hii unaishi vile unataka na una kiburi cha kufanya jambo lolote lile kwa kisingizio cha maisha
Ila kuna siku utatamani kuishi maisha tofauti na hayo ya sasa
Utapata wito na maoni ya kuwa aina nyingine ya mtu tofauti kabisa
Utapata nafasi kubwa zaidi au hata fursa nzuri na kubwa zaidi ya ulivyo sasa
Ila kumbukumbu na matukio mengi ya nyuma yatakukwamisha!
Utatamani kufuta kila kitu, kisha kuanza upya na hutoweza tena!
Utataka hata kurudisha siku nyuma na uanze upya, Ila hutoweza tena!
KUMBUKA :
Tamaa za muda mfupi zinaweza kukupa maradhi ya kudumu
Tamaa za muda mfupi zinaweza kukupa kilema na alama za kudumu
Tamaa za muda mfupi zinaweza kuvunja heshima yako ulioijenga miaka mingi sana
Tamaa za muda mfupi zinaweza kukutoa kwenye fursa kubwa za maisha yako
Tamaa za muda mfupi zinaweza kukufanya ufungwe kifungo cha maisha
Bila kusahau tamaa hizo hizo zinaweza ondoa uhusiano wako mzuri na watu wako wa karibu
Na vile vile tamaa za muda mfupi sana zinaweza geuza maisha yako kichwa chini miguu juu kwa muda mfupi mno!
Bila kusahau kukuachia kumbuka za kudumu kwako na wanao kuzunguka!
Hivyo chunguza mara mbili maamuzi unayotaka kufanya kabla hata hujachukua hatua
Usikubali tamaa ziwe chanzo cha majuto kwenye maisha yako
Usikubali kupelekwa kasi na tamaa ambazo unaweza kujizuia kwa sekunde chache tu na kutunza utu wa milele
Wala usikubali maamuzi yako mwenyewe yawe sababu ya kujuta maisha yako yote yaliyobaki
Jizuie na jishikilie kidogo, ufundishe moyo wako kuchagua kipi muhimu na kipi chakupuuza.