
Kama huwezi kujenga kabisa, basi angalau Usibomoe
Kama huwezi kutengeneza kabisa, basi usiharibu
Kama huwezi kurekebisha, basi usichokonoe
Kama huwezi kujenga hoja, basi usipinge hoja za wengine
Kama huwezi kusambaza nguvu chanya basi angalau usisambaze nguvu hasi
Kama huwezi kuleta furaha kwa watu basi angalau usiwe chanzo cha huzuni zao.
Mambo unayofanya leo hii yana mchango gani kwa wengine!?
Matendo yako ya leo, ni kwa kiasi gani hujenga au kubomoa jamii?
Njia unazotumia kupata pesa, zinajenga au kubomoa jamii?
Maudhui unayoweka mitandaoni, yanajenga au yanabomoa vizazi vya sasa na baadae?
Maneno unayotamka kwenye kichwa chako, yana jenga au kubomoa jamii?
Usiwe mbinafsi sana na kufikiria upande wako pekee
Usiwaze faida yako na ukoo wako kisha ukasahau jamii inayokuzunguka
Kama huna aibu na umeamua kujitoa kufanya unachofanya kwa lengo lako na ndugu zako basi angalau pia kumbuka jamii inayobaki na kudhurika kupitia wewe!
Shida sio njaa ya mafanikio, pesa, Mali au hata umaarufu, shida ni kwa kiasi gani utahusika kubomoa wengine kupitia njia unazotumia kupata unavyotaka
Usiwe chanzo cha majonzi kwa wazazi, ndugu na jamii inayoharibikiwa vizazi vyao kwa sababu ya njia zako Unazopita kutafuta mafanikio
Ni rahisi sana kuharibu vilivyo jengwa na ngumu sana kujenga vilivyoharibika
Leo upo na kesho haupo je mbali na Mali ulizochuma, umaarufu uliopata na mengine yote, unahisi utaacha kumbukumbu gani nyingine yenye mchango Chanya kupitia maisha uliyoishi kwenye jamii yako?