Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Kimtokacho Mtu Mdomoni Mwake, Ndicho Kilicho Mjaa

Huwezi kuingia kwenye akili ya mtu kisha kufanya uchunguzi na kujua mawazo yake

Ila kupata picha halisi kuhusu mtu huyo unaweza kupima kupitia matendo yake

Kwa sababu siku zote mtu hufanya kadiri ya mawazo na akili yake ilivyo!

Hivyo ukitaka kujua mawazo yaliyo ndani ya akili za mtu basi chunguza maneno yake

Ukitaka kujua uwezo wa mtu wa kufikiri basi angalia maneno yake

Ukitaka kuelewa mtu fulani anawaza nini kuhusu wewe, chunguza kauli zake,

Siku zote mtu hutokwa na kile kilichomjaa kwa ndani yake

Ni vigumu sana kuwa tofauti kwa nje kuliko ulivyo kwa ndani

Mtu yoyote hutenda sawa na kile anachowaza kwa ndani

Na ndio maana tunasema umasikini huanzia akilini

Umasikini wa mtu na maisha anayo ishi ni matokeo ya namna anavyofikiri kwa ndani na kwenye akili na mawazo yake.

Namna akili yako inavyo fikiria kwa ndani ndivyo utakavyotenda kwa nje

Ni mara chache sana mtu kwenda kinyume na mawazo yake

Na mara kadhaa mtu huweza kudanganya au kufeki uhalisia japo huwa hawezi kudumu kwenye hilo!

Ni mara chache sana mtu kutenda tofauti na mawazo yake yalivyo

Kwa sababu ndani ya mtu ndio huumba na kujenga nje ya mtu.

Ili kuweza kubadili mfumo wa maisha yako kwa nje, ni lazima ubadili namna unavyo waza kwa ndani

Ili kuwa bora kwa nje basi lazima uanze kuwa bora kwa ndani.

Watu wengi waliokosa hekima na busara kwa nje, mara nyingi ndani yao ndivyo walivyo!

Usitafute mchawi wala kuamini utetezi wa neno “ilikuwa bahati mbaya” hususani kama jambo limejirudia zaidi ya mara 2

Amini kuwa mtu huyo kwa ndani ndivyo alivyo na ndivyo mawazo yake yanavyo mtuma!

Elewa kuwa hakuna muujiza wa ziada kwenye ndani na nje ya mtu pia kuweza kuishi na watu vizuri ni lazima kuzingatia sana matendo yao

Kwakuwa matendo ndio hukupa ishara kujua alivyo kwa ndani na jinsi ya kwenda nao sawa!

Ukipenda sana kusoma au kuangalia aina fulani ya vitu, ndivyo ambavyo utaviishi kwa nje

Ukipenda sana kusikiliza na kujazwa aina fulani ya maongezi basi pia ndivyo utaishi kwa nje

Hivyo kabla huja teseka sana kujenga maisha ya nje ya mwili wako, anza kujenga maisha ya ndani ya mwili wako kwanza

Kabla hujachukia umasikini wako, anza kuchukia mawazo yako

Kabla hujalinganisha maisha yako na wengine, anza kulinganisha akili na mawazo yako na yao!

Na hapo utapata jawabu au namna ya kuanza kubadili maisha ya nje ya mwili wako kupitia unayoyajaza kwa ndani.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kama Huwezi Kujenga, Basi Angalau Usibomoe

Next Post

Ukitupacho Wewe Kwa Wengine Ni Dhahabu, Kumbuka Wenye Shida

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.