
Moja kati ya jambo kubwa zaidi nililojifunza hasa katika maisha ya utafutaji ni
Kuchanganya akili zangu binafsi kwenye akili za wengine
Kuchanganua mambo ninayoambiwa na wengine kabla ya kuamini
Kutokukurupuka na kuamini jambo lolote kabla ya kuchunguza
Kutokuwa kihere here kwenye mambo ninayo ambiwa
Hususani kwenye jambo linalohitaji pesa au linaloenda kuharibu uhusiano wangu kwa wengine.
Kuna watu ni mabingwa sana wa kudanganya wenzao kwa kisingizio cha mjinga ndio aliwao!
Ujinga wako kwenye kitu fulani huwa baraka kwa wengine wapigaji!
Dunia imebadilika sana kila mtu yuko bize kunufaika binafsi bila kujuli maumivu wanayoacha kwa wengine
Hawaoni shida kabisa kuumiza akili, mahusiano na mfuko wa mtu mwingine kwa manufaa yao binafsi
Watakulaghai kwa maneno yenye matumaini makubwa sana na kivuli feki cha mafanikio yao ili uingie mkenge kisha wakulize na kukimbia
Hivyo umakini unahitajika sana hasa pale unapotafuta taarifa kuhusu kitu
Umakini ni muhimu sana hasa pale unapopewa taarifa kuhusu kitu
Umakini ni lazima kwa jambo lolote lile ambalo linatoa pesa yako mfukoni au kuharibu uhusiano wako kwa wengine
Usiwe mtu unae sikiliza na kuamini haraka kila unachosikia au kuona bila uchunguzi
Tenga muda wako kufikiri na ukiweza chunguza zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote hata kama umeletewa ushahidi mezani.