
Huwa napata kigugumizi sana napoona mtu yupo tayari kutumia pesa za biashara yake kufanya matumizi binafsi lakini kamwe hawezi tumia pesa zake binafsi kukuza biashara yake!
Siku zote lazima ukubali kuumia biashara yako, kabla biashara haijaanza kukuhumia wewe!
Kama una kazi na kipato nje ya biashara unayofanya basi unapaswa kuwekeza kwenye biashara yako wakati bado changa
Kama ambavyo unajihudumia wewe binafsi kwa kipato chako binafsi, ndivyo unapaswa kuhudumia biashara yako!
Njia rahisi zaidi ni kubadili aina ya vipaombele binafsi na kuacha baadhi ya matumizi mengine kisha kuelekeza pesa kwenye biashara kwanza kwa muda maalumu
Biashara inataka matunzo ili iweze kukua na kustawi
Biashara inataka uwekezaji ili iweze kukulipa zaidi
Biashara inataka heshima nayo pia itakuheshimu mbeleni.
Mtu pekee anaeweza kujua uchungu wa biashara yako, ni wewe mwenyewe
Mtu pekee anaeweza kutunza na kustawisha biashara yako, ni wewe mwenyewe!
Mtu pekee anaeweza kuokoa biashara yako, ni wewe mwenyewe.
Fanya ufanyavyo lakini hakikisha kuwa unaijali, kuthamini na kuwekeza kila ulichonacho kwenye biashara yako
Biashara ikitunzwa vyema, itanawili na ikinawili itavutia zaidi kisha itakulipa mbeleni
Gharama zote unazotoa leo hii mfukoni kwako kwa ajili ya biashara yako, kuna siku zitakulipa zaidi kupitia faida au uzoefu!
Usiogope kujitoa muhanga kwa lengo la kukuza biashara yako
Kwa sababu ikitokea umepata na kubutua utasahau kila shida, na ikitokea umekwama utajifunza pakubwa, jambo la msingi ni hutotoka patupu!
Tumia sehemu ya mshahara wako weka kwenye mahitaji muhimu na mapungufu ya biashara yako mara kwa mara mpaka pale biashara itaanza kujiendesha yenyewe
Biashara ikianza kujiendesha ndio utaona malipo yake rasmi
Kwani gharama zako zote zitarudi na itasapoti maisha na kipato chako.