
Sio kila unacho kiona kwa macho yako ya nje, basi ndivyo kilivyo kwa ndani,
Sio kila unalo sikia kwenye masikio yako au kuambiwa na watu tofauti na wahusika halisi, basi ndivyo kilivyo
Kuna mambo mengi sana huonekana kwa namna nyingine kwa nje lakini kwa ndani uhalisia upo tofauti kabisa.
Hivyo busara ni kuuliza kwa watu sahihi na wahusika wa jambo lenyewe ili kujua ukweli halisi kama una lengo la kufahamu!
Na kama huna lengo, nia au pengine huna umuhimu na ulazima wa kujua basi busara zaidi ni kukaa kimya.
Watu wengi sana wamejiingiza kwenye matatizo yasiyo ya lazima kisa kufuata mkumbo,
Kuna wengine wanatumia muda wao mwingi kufuatilia mambo yasiyo wahusu kabisa, muda ambao wangetumia kuboresha maisha yao!
Matokeo yake hujikuta wanapata changamoto ambazo hawakupaswa kabisa kuzipata kisa umbea!
Kuna mambo mengi sana hapa Duniani huonekana ya ajabu sana kwa nje, Ila kwa ndani yapo Sawa kabisa,
Kuna vitu hupakwa ubaya kwa nje, Ila kwa ndani ni vizuri sana!
Kuna vingine vipo sawa kabisa kwa ndani au kwa wahusika halisi tofauti na uvumi ulivyo kwa nje!
Lakini pia yapo yale ambayo hueleweka kwa wale wanaopaswa kuelewa pekee, na hayana maana kabisa kwa wasio husika!
Hivyo kama ukiona kitu kina ulazima mkubwa wa wewe kujua ukweli basi uliza kwa wahusika wenyewe
Ukiona jambo lina maana kwako na ungependa kulijua kwa undani, basi pia uliza wahusika halisi
Ukihisi hali ya mtafaruku kwenye akili yako kuhusu kitu fulani, basi pia usiache kuuliza wahusika halisi
Na ukiona hayana maana kwako, hayana faida wala kukuingiza chochote basi ni bora kuacha kama yalivyo
Kwa sababu pili pili ya shamba hupaswa kumuwasha bwana shamba.