Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Anae Kucheka Leo Mpe Kiti Akae Kabisa Aendelee Kucheka Vizuri Huku Anangoja Kesho Yako

Mjomba wangu aligeuka kituko kwa watu wengi alipo amua kurudi shule kusoma upya baada ya kuona umuhimu wa Elimu aliyo ichezea zamani!

Sababu kubwa ya watu kumcheka sana ilikuwa umri mkubwa aliokuwa nao wakati ule,

Hakika alikatishwa sana tamaa hata wazazi wake (babu na bibi) walimkataza sana na kumuonea huruma.

Mjomba alikuwa na umri zaidi ya miaka 30 hivi mbali na umbo lake kubwa kimuonekano (alikua bonge na mrefu sana)

Hakika alikuwa mkubwa hata kwa macho ya nje kwa kila aliye mtazama!

Ila alipiga moyo konde licha ya kuchekwa sana nyumbani, mitaani na hata shuleni bado hakuacha kusoma.

Alianza kidato cha kwanza, uzuri shule ilikuwa private (ipo kigoma ujiji buzebazeba inaitwa Ah-lal byte) kama sijakosea,

Pale wanapokea mtu yoyote anaeweza kulipa ada tu kama ilivyo shule zote za watu binafsi.

Hivyo mjomba wangu alisoma kwa bidii kubwa sana tena kwa mateso ya kuchekwa na kudharaulika mno,

Hata mimi nilikuwa mmoja kati ya watu waliocheka sana na kumuita Baba wa darasa! Kutokana na umri wangu mdogo niliokuwa nao kipindi kile, niliona mjomba kapotea sana.

Baada ya kumaliza kidato cha nne, mjomba hakufanikiwa kwenda kidato cha tano, Ila alipata alama za kumuwezesha kujiunga chuo cha Ualimu.

Hivyo alienda kusoma Ualimu wa shule ya msingi na baada ya Kuhitimu tu alipata kazi ( miaka ya nyuma kazi za ualimu zilikuwa rahisi sana kupata).

Hivyo mpaka sasa mjomba wangu ni Mwalimu, ana maisha mazuri kiasi na familia yake imara, kiufupi ana kipato cha uhakika.

Wote ambao walimcheka hasa baadhi ya ndugu zake bado wako vile vile mpaka leo!

Maisha yao ya kuunga unga na wala hawana kipato cha maana na hata hatua zozote kubwa walizopiga.

Aibu imerudi kwao na kikubwa walichobaki nacho ni majuto kwenye mioyo yao (maana mjomba aliwashawishi sana kurudi shule pamoja nae Ila walikataa)

Mjomba alikubali kuteseka miaka 6 mpaka 7 Ila amepata faida milele..

Mjomba alikubali maumivu ya muda mfupi sababu alijua faida ya baadae,

Mjomba hakukubali kukatishwa tamaa wala kusikiliza maneno ya watu kabisa kwa sababu alijua nini anataka.

Leo amesahau kila kitu cha nyuma na anakula faida ya maamuzi yake.

Usisikilize maneno ya watu, kama una kitu kwenye akili yako na unajua faida ya kile unachofanya basi usiogope kabisa kukaza roho na moyo kwa ajili yako wewe mwenyewe.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Uliza Ujue Ukweli, Sio Kila Jambo Lipo Kama Unavyoliona Au Kulisikia Kwa Wengine

Next Post

Huhitaji Kuwa Bora Na Mkalimilifu Ili Kuanza, Anza Hivyo Hivyo Ulivyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.