
Hivi unajua kuwa Kutangulia kwako kabla ya wengine sio sababu ya kufika kabla ya wengine?
Hivi unajua kwamba Kutangulia kwako kabla ya wengine sio sababu ya kupata wa kwanza kabla ya wengine?
Simaanishi kuwa kuchelewa ni kigezo cha kuzingatiwa au kizuri
Na wala simaanishi kuwa hutakiwi kuwahi kufika kabla na unapaswa kuwa nyuma
La hasha!
Nina maanisha kuwa haijalishi umewahi Kutangulia umbali gani kuliko wengine, hio sio sababu ya wengine kuwa nyuma daima
Haijalishi utapata vingapi kabla ya wengine, elewa kuwa nao muda wao ukifika wanaweza kupata kuliko wewe
Haijalishi umepata mafanikio kiasi gani kabla ya wengine, jua tu hata wao wanaweza kupata mwishoni kwa kuchelewa sana Ila wakapata kilicho bora kuliko chako.
Hivyo unapotangulia mbele ya wenzako isiwe sababu ya kujiona mjanja au umepatia sana maisha
Unapopata nafasi ya kuwa mbele ya wenzako usijione mjanja sana na tayari mwendo umeumaliza!
Unapopata baraka yakuwa mbele kuliko wengine, elewa kuwa hata wao kuna siku watafika na hata kukupita umbali zaidi ya uliopo wewe
Hivyo heshimu sana yule unaemuacha nyuma haijalishi umemuacha umbali kiasi gani
Maisha hayapo kwa ajili ya mtu mmoja bali yapo kwa wote wanao yatafuta
Halafu uzuri wa maisha ni kuwa hayana bajeti, (budget) yaani yenyewe hugawa kwa yoyote wakati wowote na hayajawahi kuishiwa!
Hivyo kuwa makini sana na usihisi kama umemaliza budget ya maisha na wengine hawawezi kupata tena
Kwa sababu kuna siku unaweza kushuka chini ukakosa hata mahala pa kuomba msaada
Waswahili wanasema “usitukane mamba kabla hujavuka mto”