Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Hivyo Unavyojihisi Ni Sawa Ila Pia Unapaswa Kuendelea

Kuna muda mambo huwa magumu sana kiasi hutamani kupata mtu wa pembeni,

Mtu ambae atakwambia usijali kila kitu kitakaa sawa…

Mtu ambae atakutia moyo na kukupa sapoti hatua kwa hatua…

Mtu ambae atakunyamanzisha pale unapohisi kulia..

Mtu atakae kutua mzigo mzito wa mawazo pale unapohisi kuelemewa..

Najua na ninaelewa sana mambo sio rahisi kama yalivyo

Ila kumbuka hakuna mtu jasiri nyakati zote,

Hata yule unae muona jasiri sana na unamchukulia kama mfano wako wako wa kuiga,

Elewa na yeye kuna muda huzidiwa na hata kutamani kuacha anachofanya!

Maisha yana changamoto nyingi sana tukiondoa changamoto kuu ya kukosa kipato.

Changamoto zote za kila aina hufanya watu kuhitajiana, kufarijiwa na kupewa hamasa zenye kuleta nguvu mpya.

Sasa unapokosa mtu huyo wa pembeni, hupaswi kukata tamaa moja kwa moja

Hupaswi kuishia hapo ulipo wala kuona huwezi kuendelea tena,

Bali unapaswa kugeuza mtu unaemtaka kuwa wewe mwenyewe binafsi..

Jifanye wewe ndio yule mtu ambae ungetamani awe karibu yako wakati wa magumu unayopitia

Jipe moyo na jifariji kwa namna yoyote ile unayoweza

Jiambie maneno mazuri na yenye kukupa hamasa mara kwa mara

Sio rahisi lakini tambua kuwa inawezekana!

Mfano mimi binafsi mara kadhaa ninapozidiwa na kukosa mtu wa karibu yangu, hujiambia

(Mwajuma wewe ni jasiri sana, una nguvu na uwezo wa kushinda kila jaribu

Mwajuma najua umechoka sana na hili ni zito kwa upande wako Ila unaweza kufanya tena na kumaliza kwa ushindi

Mwajuma ulipotoka ni mbali sana hivyo usikubali kuishia hapo ulipo

Mwajuma yote unayopitia ni sawa kabisa na kwa sababu una malengo makubwa na lazima uyatimize

Mwajuma simama sasa nenda kwa ujasiri na maliza kila ulichokiacha).

Sio hivyo tu, kila siku ninapo kutana na jambo lenye kunivunja moyo au gumu zaidi huwa ninajiambia

“it’s okay everything will be fine and I can do it”

Hayo maneno ni madogo sana Ila yana nguvu kubwa mno kwenye nyakati ngumu.

Zoea mara kwa mara kujiambia maneno ya kishujaa pale unapohisi kuelemewa

Tambua kuwa hata kama utakuwa na mtu wa pembeni, kuna wakati hato kuwepo,

Hutokuwa nae daima na hawezi kukupa moyo mara zote (watu huja na kuondoka)

Hivyo wewe binafsi unapaswa kusimama kwa ajili yako, ndoto na malengo yako.

YOU CAN WIN IF YOU WANT

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Urafiki Wa Kweli Hauna Mashaka Wala Kipimo Cha Upendo

Next Post

Bora Ujaribu Ukose Kuliko Kuacha Kujaribu Kabisa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.