
Kulalamika kwenye mambo ambayo unapaswa kuwajibika nayo ni miongoni mwa vitu vinavyoongeza ugumu wa jambo lenyewe!
Haijalishi hata kama ni kweli una haki ya kulalamika,
Hata kama umeonewa sana na hukupaswa kufanyiwa unachofanyiwa
Bado kulalamika sio suluhisho la matatizo yako kamwe
Kuna njia 2 mbili zakufanya kama unahisi hustahili hicho kitu
- Acha kabisa kufanya, kaa kimya na jiondoe kabisa
- Baki na fanya bila kulalamika kabisa
Ajabu ni pale unakuta mtu anafanya huku analalamika kutwa kucha
Anafanya huku anaona kama ameonewa na hastahili kufanya
Yaani anafanya huku amejaa kisirani na jazba kubwa
Sasa mbaya zaidi ni pale kitu anachofanya kina faida kwake yeye mwenyewe!
Mfano unalalamika kazi yako mbaya lakini bado huiachi na mwisho wa mwezi wewe ndio wa kwanza kuuliza mshahara kama umeingia!
Unalalamika mahusiano yako mabaya Ila bado huachiki miaka nenda miaka rudi!
Unalalamika biashara ngumu Ila bado kila siku tunakuona unafungua duka!
Unalalamika Elimu haina maana, Walimu wanakupeleka resi wakati huo huo huachi hayo masomo!
Sasa kuna haja ipi ya kulalamika?
Au toka uanze kulalamika ulipata faida gani mpaka sasa?
Tangu uanze kulalamika umeshawahi kuona muujiza kupitia malalamiko yako?
Kama jibu ni ndio basi endelea kulalamika tu..
Na kama jibu ni hapana basi hupaswi kamwe kulalamika,
Badala yake hio nguvu unayotumia kulalamika iongeze kwenye utendaji wa hiko kitu
Kama huwezi kuacha moja kwa moja maana yake, hilo jambo lina faida na wewe!
Hivyo unapaswa kuzidisha nguvu kulifanya badala ya kulalamika unayopitia
Elewa kuwa kila kitu kina changamoto zake na hizo unazopita ndio changamoto za jambo lako
Zikubali na nenda nazo sawa huku ukitafuta namna ya kuzizoea au kuzipunguza.