
Kuna wakati utakuwa na nguvu ya mwili kubwa sana na kuna wakati nguvu hio itaisha kabisa
Kuna muda utakuwa mzima wa afya nzuri sana na kuna muda afya inaweza kupotea kabisa
Kuna kipindi utakuwa na muda mwingi sana halafu kuna kipindi utakosa muda kabisaaaa.
Hivyo ni vyema kutumia vitu hivi vitatu kwa akili, maarifa na busara kubwa ili kuepuka majuto baadae,
Ubaya wa muda ni kuwa haurudi nyuma na kadiri muda unavyo kwenda ndivyo nguvu na umri hupungua taratibu na mwisho kufika ukingoni!
Mzee ambae unamuona leo hii, namna alivyokongoroka na kuisha kabisa, kumbuka zamani alikuwa kijana na mwenye nguvu nyingi pengine kuliko ulizonazo wewe sasa!
Kwa maana hiyo kila mara kumbuka unakaribia kuwa kama yeye na pengine usifike umri alionao kabisa.
Maisha hayana huruma linapokuja suala la umri na nguvu, hivi vitu vikipotea huwa vimepotea mazima,
Hivyo kuwa makini sana kwa muda unaopoteza leo kwasababu kuna siku utajutia sana kwa kila sekunde uliyopoteza!
Afya unayochezea leo, kuna watu wanatamani hata robo yake na hawajabarikiwa kabisa
Watu hawa wanatamani itokee muujiza wapate hata nguvu ya kusimama tu au kutoka nje kuona jua la Mungu Ila imeshindikana miaka na miaka.
Usijali sana kuhusu pesa na mali kwa sababu ni vitu ambavyo huweza kupatikana hata kama vikichelewa au kupotea!
Ila afya, muda na nguvu ndio kama Dhahabu yako ambayo unapaswa kuitumia na kuilinda kwa akili zako zote.
Kumbuka hata jua huwaka sana mchana lakini huzama jioni!
Umri, muda na nguvu ni kama uonavyo jua la mchana, hivyo vitumie kwa akili na busara ya hali ya juu mno.
Lifewithmuhasu.com