Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Aliyekataa Kulima Na Wewe, Hafai Kula Pamoja Na Wewe

Kuna watu hujitenga mbali sana wakati wa kulima na maandalizi ya shamba

Halafu huja mapema mno wakati wa mavuno unapofika!

Hawa ndio wale ambao wanapoona wenzao wanateseka kuandaa maisha ya kesho hufanya kama hawaoni kabisa,

Hawaishii kwenye kujifanya hawaoni bali huweza hata kucheka na kudharau harakati ndogo za wenzao na hata kuona hazina maana!

Mambo yanapokuwa mazuri mbeleni, sasa ndio huja na kutaka faida kupitia mgongo na nguvu za wenzao,

Kosa ni pale wanaponyimwa ndio hueneza chuki na visasi vya kila aina kila mahala.

Nakumbuka wakati naanza kampuni yangu ya Muhasu Domestic Helpers Agent nikiwa mwaka wa mwisho chuoni,

Nilihitaji watu ambao nitasaidiana nao kuanzia chini kabisa kwenye vitengo mbali mbali.

Moja kati ya watu ambao nilitamani sana kufanya nao kazi alikuwa rafiki yangu niliyejuana nae wakati nasoma pale Hekima upland (nilisoma advance kama mtahiniwa wakujitegemea)

Huyu dada nilizoeana nae pale shuleni na bahati nzuri tulifaulu pamoja kwenda chuoni mkoa mmoja ila vyuo tofauti kwahio hii iliongeza zaidi ukaribu wetu na kujuana zaidi.

Bahati mbaya nilikosa mkopo na kurudi dsm ila yeye alibahatika kulipiwa ada na ndugu zake,

Hivyo wakati mimi nikiwa mwaka wa mwisho chuoni tayari yeye alikuwa mtaani baada ya kuhitimu ila hakuwa na kazi.

Hivyo niliona ni fursa nzuri sana kwa yeye kuja kuanza biashara pamoja nami angalau kwa ujira mdogo kuliko kukaa nyumbani bila kazi kabisa,

Kweli alikuja kuona ofisi yangu ilikuwa na wiki moja tu toka nifungue pale na hata ilikuwa haina vitu vya thamani ndani.

Baada ya kumpa maoni yangu na kutaka aje tupambane pamoja kukuza kampuni ajabu ALIKATAA KABISA

akasema kwa namna anavyoona hatoweza, nikauliza sababu “akadai mshahara mdogo” (ilikuwa 150k kula na kulala juu yangu maana nilikuwa na chumba karibu na ofisi pale so nikaona sio shida tukikaa pamoja kupunguza gharama za maisha upande wake.

Nilishangaa alipokataa, ukizingatia sisi ni watu wa karibu na wote tunapambana na maisha lakini pia hana kazi kabisa zaidi ya kulala ndani!

Nilimuomba sana ila akasema eti “Mwajuma, pambana kwanza kampuni ikue kuwe kwanza halafu ndio ntakuja”

So nikapata jawabu kuwa amedharau mwanzo wangu mdogo!

Kumbe shida sio mshahara ila ni muonekano wa ofisi na mwanzo mdogo wa biashara yangu!

Ukweli niliumia sana, sio kwakuwa amekataa ila nilidhani rafiki wa karibu anaweza kunipa moyo na maoni ya mbali badala yake alidharau mwanzo wangu.

Sikuwa na jinsi nilikubali na kuacha aende.

Nilipata watu wengine ambao tukaamua kupambana na biashara na Mungu hakutuacha nyuma kweli biashara ilipata jina ndani ya mwaka mmoja tu!

Nikapata wateja wengi sana na hata kufungua branch dodoma (kulikuwa na wateja wengi pia waliotaka huduma ya wafanyakazi wa ndani dodoma).

Baadae sana yule dada alinitafuta alipoona biashara inaenda nafanya matangazo mpaka redio na TV mbalimbali (nilikuwa naitwa kufanya interviews za wadada wa kazi),

Akaniomba aje kufanya kazi na mimi NILIKATAA na huo ukawa mwanzo rasmi wa chuki kubwa kati yetu

Alinichukia sana na kutangaza nimenyima kazi, akasema nina roho mbaya na sina urafiki wa dhati!

Hakika niliumia ila sikujali kwa maana nilimuona kama mtu aliyekosa dira ya maisha tu kwa sababu awali alikataa kuanza na mimi chini na sasa anataka kula matunda yakiwa juu!

Nilikuja kuacha ile biashara kwa sababu za nje ya uwezo wangu kwa baadae sana,

Ila mpaka sasa ni moja kati ya biashara ambayo sio tu ilinipa uzoefu na koneksheni za watu pekee bali pia ilisaidia wadada wengi sana kujua haki zao za kazi za ndani na kuongeza thamani ya viwango vya mshahara kwa wafanyakazi wa kazi za ndani Tanzania na ninajivunia sana kwa hilo mpaka leo.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Nguvu Ni Kama Jua, Huwaka Sana Mchana Lakini Huzama Jioni

Next Post

Uhai Unatosha Kukupa Sababu Ya Kuishi Kama Wengine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Jifunze Kushukuru

Kadiri unavyo shukuru Ndivyo unavyojisogeza karibu na mafanikio yako Jifunze kuwa na moyo wa kuyaona mazuri…

Huruhusiwi ku copy makala hii.