Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Uhai Unatosha Kukupa Sababu Ya Kuishi Kama Wengine

Tengeneza njia yako unayoweza kupita na kufika mahala unapotaka wewe mwenyewe binafsi,

Kama maisha hayajakupa njia unayotaka basi pia utapaswa kuandaa njia yako wewe mwenyewe unayotaka!

Kuna watu huzaliwa wakiwa na njia zao..

Kuna ambao hutengenezewa njia na wapendwa wao..

Kuna wale ambao maisha huwapa surprise ya njia bila kutarajia…

Halafu kuna mimi na wewe ambao hatupo kwenye kundi lolote kati ya hayo!

Kuna sisi ambao tukiacha kuandaa njia zetu basi hatuna wakumkomoa zaidi yetu wenyewe,

Sisi tuliozaliwa kama bahati mbaya tu, halafu tunapaswa kuishi kwa makusudi! (tunapaswa kujipambania)

Hii ndio tunaita struggle for the fittest

Sisi ambao Mungu na maisha yake kwa ujumla aliondoa kila kitu kwetu lakini bado tunapaswa kuishi kama walivyo wenye kila kitu!

Mungu aliondoa kila nyezo iliyo karibu yetu na kututaka tuishi kama walivyo wengine!

Sisi ndio wale ambao hatuna kimbilio tegemeo wala tumaini lolote kutoka kwa yoyote zaidi yetu wenyewe!

Sisi ambao tukilia, tukicheka na hata tukiweza au kukosa bado hatuna yoyote karibu yetu anaeweza kuhisi maumivu wala hisia zetu zaidi yetu wenyewe!

Licha ya yote hayo bado tunapaswa kuishi kwasababu tumepewa zawadi ya uhai ambayo wengi sana wameikosa!

Kuna wenye pesa na mali nyingi sana lakini wamekosa uhai!

Kuna wenye vyeo na madaraka makubwa sana ila wamekosa uhai!

Kuna wenye Falme na koo kubwa sana ila hawana uhai!

Licha ya uwezo wa kumpa Mungu kila wanachoweza ili kubaki hai, Lakini uhai haukuwapa nafasi ya kubaki upande wao!

Hivyo tunagundua kuwa pesa, mali, watu etc ni muhimu sana kwenye maisha yetu lakini vyote havina maana kama hauna uhai!

Tuendelee kutengeneza njia zetu tukiamini kuwa licha la kukosa vyote kama wengine tuwaonao! Bado tuna uhai sawa na huo walionao!

Tuamke, tujikongoje, tujivute, tujisukume na tuishi maisha kwa kufurahia uhai wetu wakati tukiandaa njia zetu!

Kwakuwa Mungu ametuumba kama wengine, katupa uhai kama wengine basi hio pekee inatosha kuwa sababu ya kujiamini na kujipambania kwa jasho na damu mpaka mwisho.

Acha kulia, acha kuumia, kumbuka una thamani sawa na mwingine yoyote yule mwenye uhai sawa na wewe, pesa na mali isiwe sababu ya kuwa mnyonge TENGENEZA NJIA ZAKO.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Aliyekataa Kulima Na Wewe, Hafai Kula Pamoja Na Wewe

Next Post

Maisha Yakikuzidi Mwendo, Geuka Nyuma Angalia Umbali Uliotoka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.