Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Maisha Yakikuzidi Mwendo, Geuka Nyuma Angalia Umbali Uliotoka

Kuna muda unapaswa kugeuka nyuma yako kisha kuangalia ulipo,

Wakati unageuka nyuma chunguza umbali kiasi gani umetoka mpaka kufika hapo ulipo sasa! Bila kujali mwendo unaotembea…

Ukishagundua umbali huo basi inatosha kukupa sababu ya kufurahi sana au kulia sana kisha baada ya hapo utajua kwa namna gani unapaswa kuongeza au kuboresha jitihada zako za safari!

Furaha ya safari yako wakati mwingine huchangiwa na kujua umbali uliotoka nyuma yako!

Kuna muda unaweza kuhisi hujafanya chochote kwasababu unaangalia ulipo kwasasa pekee!

Ila ukigeuka nyuma kisha kuvuta picha halisi ya mabonde, milima au hata tambarare ulizopita mpaka hapo ulipo basi itakufanya upate nguvu mpya ya kumaliza safari yako.

Haijalishi ni kweli bado upo mbali sana kufikia tamati, lakini kumbuka ulipotoka!

Kabla hujasema wewe si chochote, kabla hujajilaumu na kuona kama huna ulichofanya!

Basi angalau jipongeze kwa umbali huo huo mdogo uliopo sasa hivi!

Inawezekana kweli umetumia nguvu kubwa sana na huoni matokeo yoyote yale, lakini kamwe ninaamini haupo kama ambavyo ungekuwa kabla hujaanza safari kabisa!

Mafanikio hayohayo madogo kwa sasa bado yanakupa utofauti mkubwa sana na jinsi ulivyokuwa kabla hujaanza!

Angalau mara moja moja jisemee kuwa wewe ni jasiri sana kwa maana umefika mahala ambao wengi walishindwa kufika!

Usijali kuhusu umbali uliobaki, zingatia kule ulipotoka kisha amua kujipa pongezi wakati unapanga mipango ya kumaliza safari yako.

Uzuri wa maisha ni kuwa hayana haraka! Yenyewe huendelea na safari yake lakini kamwe hayafiki wala kusimama…

Hivyo haijalishi utayafata kwa mwendo gani, bado unaweza kuyafikia, kutimiza vigezo vyake kwa kadiri ulivyokusudia kisha yenyewe hukupa kwa kipimo kinachokufaa baada ya kukagua vigezo na masharti!

Kwa maana kuwa hata uchelewe miaka 50, ukitimiza vigezo vinavyotakiwa tu basi maisha yatakupa kulingana na vigezo vyako!

Hivyo usiogope sana kuhisi umechelewa au umeachwa umbali mrefu

Usijione mjinga sana au kujishusha thamani yako kisa kuwahi maisha…

Usikimbizane na maisha sana ukasahu kuyaishi maisha yenyewe!

Usikose raha wala amani ya moyo kwa sababu ya maisha

Usijilinganishe na wengine walio umbali mrefu zaidi yako!

Nenda kwa mwendo wako, furahia safari yako na kisha jipongeze kwa namna yako wakati ambao unangoja kutimiza vigezo vyako ili maisha yakupakulie kipimo chako!

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Uhai Unatosha Kukupa Sababu Ya Kuishi Kama Wengine

Next Post

Kurudisha Mpira Kwa Kipa Kwenye Utafutaji Ni Kama Matumizi Ya Boya Baharini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.