
Jisamehe wewe mwenyewe kwanza kwa makosa mengi uliyo jikosea zamani
Jisamehe kwa kosa la kuishi kwenye maisha ya watu wengine wasiokupenda na kuona thamani yako
Jisamehe kwa kutojipa kipaombele na kuwapa wengine kwa lengo la kuwafurahisha
Jisamehe kwa kujiacha nyuma, kutofurahia pesa zako na kujifurahisha kwa sababu ya watu ambao leo hii hawajakulipa wema wowote
Jisamehe kwa ahadi zote ulizojipa lakini ukashindwa kabisa kuzitekeleza wewe mwenyewe kwa sababu yoyote
Jisamehe kwa kupoteza muda kufuatilia mambo ambayo hayaja kujenga mpaka sasa wala kukusaidia chochote
Jisamehe kwa mipango yote uliyopanga kwa ajili yako lakini ukaishia njiani kisa kutoona matokeo mapema
Jisamehe kwa malengo yote uliyoweka Ila bila sababu yoyote ukagairi kuyatekeleza
Jisamehe kwenye kila kitu hata kama hukusababisha wewe au kuna sababu za msingi sana zilikukwamisha
Ukimaliza kujisemehe jiambie kuanzia sasa
SITOKUBALI KURUDIA MAKOSA YANGU TENA
Kisha anza upya ukiwa na imani na nguvu kubwa moyoni
Na wakati huu fanya kweli huku ukiogopa kurudia yale yale uliyoyafanya zamani
Rekebisha maisha yako kwa kuanza na wewe mwenyewe kabla ya kulaumu wengine.