Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Bora Ujaribu Ukose Kuliko Kuacha Kujaribu Kabisa

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kufanya kisha kukosa na kutokufanya kabisa

Elewa tu kuwa kufanya halafu ukakosa ni bora kuliko kutokufanya kabisa

Ni bora ufanye au ujaribu na ukose kuliko kuacha kujaribu kabisa.

Kwenye maisha ya utafutaji, unahitaji kitu kimoja tu ambacho kitabadili maisha yako moja kwa moja,

Ili kukipata kitu hicho basi unapaswa kukitafuta katikati ya vitu vingine vingi

Na kukitafuta katikati ya vingine maana yake ni kujaribu hiki na kile mpaka upate kilicho chako!

Moja kati ya njia ya kukipata hiko kitu ni kujaribu hata hicho kinacho kutia uvivu sasa hivi!

Huwezi jua labda hiko cha sasa ndio kikawa kile unachopaswa kuwa nacho na kubadili historia yako yote!

Simama nenda muda huu, Jaribu na usiogope kushindwa

Nenda kajaribu na usiogope kukosa wala kupoteza

Kwasababu maisha humpa anae yatafuta na wewe ni mmoja ya watafutaji.

Usiseme

“nimesha jaribu sana sikupata bora niache tu maana napoteza muda”

Elewa kuwa ukiacha kabisa humkomoi mtu yoyote bali unawaongezea nafasi wengine ya kushinda kupitia nafasi yako!

Nenda jaribu, ukikosa jaribu tena na tena na tena mpaka upate.

Kama hujapata mbadala wa hiko unacho jaribu kwa sasa basi hupaswi kuacha

Kama hujaona njia nyingine ya kupita kwa sasa basi usiache kupita njia uliyonayo

Kama hujapata namna nyingine ya kukupa unachotaka basi endelea kujaribu hicho ulichonacho.

Jaribu na endelea kutafuta huku na kule bila kukata tamaa

Ukiishiwa nguvu, rudi pumzika kisha endelea tena na tena,

Acha pale unapoona sasa unaweza kutumia njia nyingine bora zaidi na kushinda kuliko hio ya awali

Usiyape nafasi maisha kusema kuwa wewe ndio mwenye makosa kutokana na uvivu wako wa kujaribu

Wala usiyape sababu maisha kukunyima inachopaswa kukupa

Nenda sasa ushindi upo kwa ajili yako.

YOU CAN WIN IF YOU WANT

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Hivyo Unavyojihisi Ni Sawa Ila Pia Unapaswa Kuendelea

Next Post

Ewe Msomi, Kama Elimu Yako Haijakupa Maana Basi Usidharau Kazi Zisizo Na Maana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Tengeneza Mabawa Yako

Usikubali mazingira yakwamishe ndoto zako wala kukupa vikwazo vya kuwa unavyojiona kwa ndani Usikubali watu…

Huruhusiwi ku copy makala hii.