
Maisha ni safari ndefu yenye kila aina ya majaribu, mitihani na changamoto
Kila jambo kwa namna yake lina changamoto zake
Hakuna kitu ambacho kitakufanya kwa asilimia miamoja uwe salama bila misukosuko kadhaa!
Kila utakacho kichagua lazima ukubali changamoto zake yani ni kama unavyopenda boga basi utapaswa kupenda na Ua lake
Kwahio chagua changamoto Chanya zinazokukuza na kubadili maisha yako huku zikukupa nuru ya kesho yako
Usikubali kukumbatia changamoto zinazokuumiza na kukupa mateso huku zinashusha thamani na maana ya maisha yako
Songa mbele ukiwa umebeba changamoto zinazokufanya uone maisha kwa tafsiri ya maana na kusudi la kuumbwa kwako
Usikubali kuwa mtumwa kwenye maisha ya watu wengine
Usikubali kutumika kwa faida za watu wengine
Usikubali kulia na kuona Dunia kama sehemu ya maumivu
Tumeletwa Dunia kufurahia kwa kila sekunde inayopita
Chagua changamoto zako hata zikikutesa bado siku moja upate ujasiri wa kusimama kwa ushindi na kusimulia wengine funzo Chanya.
#YOU CAN WIN IF YOU WANT