
Maisha unayoishi sasa kuna siku utafurahia sana au utajutia sana
Haijalishi utakuwa na mafanikio makubwa zaidi au madogo sana
Majuto au furaha hutegemea na aina ya mtindo wa maisha ambao umechagua kuutumia kupata kipato chako!
Kutokana na sababu au kiu ya mafanikio unayotaka, kuna wakati unaweza kufanya kitu chochote kile
Hutozingatia vigezo, kesho yako, sheria za Dini wala za nchi au hata maumivu unayo sababisha kwa wengine..
Vile vile hutofikiria madhara na sintofahamu za maisha ya baadae kwakua maisha huwa hayagandi na kuna siku utajikuta kwenye maisha tofauti kabisa na hayo ya sasa
Hutowaza familia au vizazi vyako vijavyo au hata jamii kwa ujumla wake
Hutowaza maumivu utakayopata baada ya akili zako kurudi na shida zako kuisha au hata zisipoisha kabisa
Kitu pekee ambacho utakuwa nacho moyoni ni kiu ya mafanikio (haijalishi unataka mafanikio eneo gani).
Aina ya watu wanao kuzunguka sasa wanaweza kukufanya upite njia yoyote ile ili tu ufanikiwe
Njaa inayokusumbua sasa inaweza kukufanya uuze utu wako kwa gharama yoyote ili tu ujaze tumbo
Tamaa ulizonazo sasa zinaweza kukufanya ufuate mkumbo wowote kwa lengo la kupata unachotaka tu
ILA
Kuna muda utafika inawezekana ukawa kweli umepata mafanikio uliyo taka au hujafanikiwa kabisa,
Kumbukumbu za matukio mabaya zitakusonga kwenye akili yako kila sekunde
Utakumbuka kila baya ulilofanya kwa sababu za kiu ya mafanikio yako
Utahisi hali ya kujuta kupitiliza haijalishi mafanikio hayo umepata au hujapata
Utatamani upotee uende mbali sana kwa maumivu na majuto ya mambo uliyofanya haijalishi yalikuwa ya siri au dhahiri kwa watu
Lazima utalipa kwa kiwango kile kile, mateso na mchakato mbaya uliopita nyuma!
Sio lazima ulipe kwa wengine waliodhurika kupitia wewe la hasha!
Malipo utayapata wewe binafsi ndani yako mwenyewe kwenye moyo na roho yako!
Na hapo utagundua kuwa mafanikio hayana maana yoyote zaidi ya kutengeza historia ya maisha yako iliyo na maana kwako binafsi, jamii na Mungu wako
Bila kusahau mafanikio yanayo ambatana na amani au furaha ya dhati ukiondoa pesa, nyumba au hata magari ya kifahari.
ANZA SASA KUBADILI NJIA ZAKO HUJACHELEWA.