
Hapa Duniani kuna mambo ya kila aina kwa kila namna
Licha ya ukubwa wa Dunia, mabara na nchi zake
Kuna watu wengi sana ambao kila mmoja kwa namna yake ana kitu tofauti na mwingine!
Kuanzia tabia, akili, mawazo na hata muonekano
Kuna mambo hufanyika kwa watu fulani ambayo ni kituko kwa wengine
Kuna yale mazuri sana kwa watu fulani lakini huonekana ya ajabu mno kwa wengine
Kuna tabia mbaya sana tena zenye kuchukiza mno kwa watu aina fulani, Ila ni nzuri mno na zinazo heshimika kwa watu wengine
Pia kuna mila na tamaduni za ajabu sana kwa mataifa fulani, Ila zinapendwa kwa mataifa mengine!
Usisahu biashara na kazi mbalimbali za watu aina mbalimbali
Kuna biashara nzuri sana na zenye faida kwa mtu fulani Ila mbaya zaidi kwa mwingine
Kuna kazi nzuri kwa mtu yule Ila kazi ile ile ikawa mbaya sana kwa mtu mwingine,
Kipato kidogo kwa mtu huyu kinaweza kuwa ndio utajiri wa mwingine!
Hivyo kamwe huwezi miliki na kufurahia kila kitu sawa na wengine!
Huwezi elewa maisha ya kila mtu kamwe
Wala huwezi lazimisha mambo yawe sawa kwa kila mtu
Hivyo unapaswa kuchagua vichache vyenye maana kwako,
Kisha vishikilie kwa mikono miwili na ishi ndani yake
Halafu vingine vyote vifanye kama sehemu ya utalii wa macho na masikio yako!
Yani ukiviona au kuvisikia basi viache hapo hapo na zingatia yako
Tofauti na hapo utachangayikiwa na kupoteza muelekeo kabisa
Utaweka roho juu na kuona Dunia kama sehemu mbaya isiyofaa au ipo kwa ajili ya wengine tu
Utakosa muelekeo wa nini ushike au nini uache, kipi uamini na kipi uache
Kwa sababu ya kutaka mambo yote hata yasiyo kuhusu au kuwa na faida kwako
Zingatia maisha yako, tafuta maana ya maisha yako na ishi kwenye njia zako
Kiufupi ya Ngoswe muachie Ngoswe