
Weka mazoea ya kuwaza mambo Chanya kila mara
Bila kujali maisha yako ya sasa wala vikwazo ulivyo navyo
Kadiri unavyowaza mambo mazuri na Chanya ndivyo unayavuta karibu yako
Kumbuka ukiwa karibu na UA ridi basi hata na wewe utanukia na ukiwa karibu na harufu mbaya na wewe utanuka!
Jinenee mambo mema kila wakati na weka imani kuwa inawezekana kuyapata
Kataa kabisa hali ya kukata tamaa na kujinenea mabaya au hata kujichukulia mnyonge na usiyejiweza
Epuka hali ya huzuni na kujiona hufai kila wakati hata kama una pitia magumu
Elewa kuwa changamoto haziepukiki Ila unaweza kuepuka namna unavyozipokea na jinsi unavyo kabiliana nazo..
Kumbuka unaweza kuwa vile unataka na kuishi maisha unayotamani kama ukiamua wewe mwenyewe
Usikubali kabisa kujiona wa kawaida wewe ni wa thamani kubwa sana.