
Jana ulisema utaanza leo
Wiki iliyopita ulisema utaanza wiki hii
Mwezi uliopita ulisema utaanza mwezi huu
Mwaka uliopita ulisema utaanza mwaka huu
Ajabu ni kuwa hujaanza mpaka leo!
Kila siku unasema utaanza Ila huanzi
Kila mwaka unasema utaanza Ila huanzi
Umeshazoea kutafuta visingizio visivyo na tija kila kukicha
Imefika hatua unaogopa kujipa ahadi mpya maana unajua kabisa kuwa hutoitimiza!
Mbaya zaidi unaogopa kutamka hata kwa wanaokuzunguka ahadi mpya kwakua unajua hawawezi kukuamini tena,
Wameshazoea ahadi na mipango yako isiyo tekelezeka!
Sasa jiulize utaishi hivyo mpaka lini? Utatafuta sababu mpaka lini?
Utaendelea kutafuta visingizio hadi lini? Au lini utapata kila kitu kitakacho kufanya uanze?
Najua huna majibu yenye tija, uzito wala mantiki kubwa,
Bali umechagua kuwa upande wa washindwaji!
Umechagua kuwa mzururaji kwenye hii Dunia
Umechagua kuwa mlalamikaji kwenye kila jambo
UNAJUA KWANINI?
Elimu Yako Kubwa Inakudanganya na kukufanya ujione wa thamani kuliko kazi na biashara unazopata!
Hebu geuka nyuma, kisha tazama yule mlemavu anavyopambania maisha yake!
Geuka tena muangalie yule mama mjane mwenye watoto zaidi ya watatu anavyopambania maisha yake
Bado tena! tazama yule Baba pale, hana elimu wala koneshkeni kubwa mjini Ila halali ndani sababu ya kutafuta mkate wa kila siku
Bado! endelea kutazama huyu dada sio mrembo kama unavyo amini, hajasoma wala hana sapoti yoyote Ila amebeba beseni la matunda kichwani anatembeza barabarani kwa ajili ya maisha yake!
Haya muangalie huyo mtoto hapo, kila siku haachi kuzunguka na mayai kichwani au karanga za kukaanga kwa lengo la kupambania maisha yake.
Sasa wewe ndugu yangu umesoma na una Elimu kubwa ya chuo Ila mpaka sasa hujaona fursa yoyote ile yakufanya!
Umekosa kazi ya Elimu yako na bado umekubali kulala ndani kisa kazi zingine sio level yako!
Elimu yako na miaka yote uliyopoteza haijakusaidia kuleta ugali mezani na bado unaona kazi za kawaida sio level yako!?!?
Leo ni siku ambayo unapaswa kujitafakari upya sasa,
Kama elimu haijakupa unachotaka, basi sasa tafuta maisha nje ya Elimu uliyonayo kwanza
Inuka nenda Jichanganye kama wengine wakati ambao unasubiri Elimu ikupe muujiza unao hitaji.
Huna sababu za kuona wengine hawana maana kama wewe pia Elimu yako haijakupa hio maana.
Maisha hayachagui mwenye Elimu wala asiye na Elimu
Bali maisha yapo kwa ajili ya mtu yoyote anae yatafuta.