Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Hakuna Tuzo Za Kelele, Unapotaka Kuondoka Kwenye Maisha Yao Basi Ondoka Kimya Kimya

Moja kati ya vitu ambavyo nimejifunza zaidi kwenye maisha yangu ni kuacha kupiga kelele wakati ambao nataka kuondoka!

Zamani nilikuwa bingwa sana kuonesha kuwa na mimi naweza kujibu pale napoona thamani yangu imeshuswa

Nilikuwa mtu ninae penda sana kujieleza au hata kugombana na mtu au watu wanao nidharau na kunishusha hadhi yangu

Sikujua kama nilikuwa nakosea sana maana sijawahi kupata faida yoyote zaidi ya kujenga uhasama wa kudumu na watu wale,

Mbali na uhasama bado chuki niliyo pandikiza ilinitesa sana kwenye moyo wangu na kujaa kisirani hata kwa ambao hawana makosa wala hawaja nikosea kabisa.

Baadae sana sikuona faida ya maisha yale hivyo niliona nijaribu kuwa mkimya tu hasa pale mambo yanapoenda nje ya matarajio yangu kwa watu niliowapa vipaombele kwenye maisha.

“KUONDOKA BILA KUPIGA KELELE”

Kuna muda maumivu huwa makali na hata kutamani kujieleza sana kwa watesi wako,

Kuna zile nyakati ambazo bado moyo wako unahitaji kuwa karibu na watesi wako

Na hata unatamani kuwapa sababu za wao kubaki kwenye maisha yako!

Inawezekana bado unawapenda sana au hata huwapendi Ila unataka jamii ijue kwa namna gani uliwapa vingi vya thamani kuliko malipo wanayokupa.

Nyakati kama hizi ndio hupelekea wengi kugombana na hata kuacha alama mbaya baina yao,

Hizi ndio zile nyakati ambazo visasi hujengwa mioyoni na maneno yasiyofutika hutamkwa bila kutarajia

Mbaya zaidi watu hujikuta wanaharibu zaidi kuliko kujenga (maana wengi huongea kwa hasira tu bila kumaanisha wanayo ongea).

Sasa kuepuka yote hayo na hata kulinda thamani na heshima yako pindi unapo choka kuona huthaminiki na mtu au watu fulani,

Basi unapaswa kuondoka kwa watu hao bila kupiga kelele kabisa.

Kupiga kelele maana yake kugombana na mtu (watu) au hata kujibu mashambulizi yao,

Hakuna ulazima wa kuaga pale unapotaka kuondoka bali ukimya wako hutosha kuwa jibu kwao.

Kuondoka sio lazima kusema kwaheri wala kuonesha ishara kuwa sasa unaondoka kwenye maisha ya mtu asiyethamini uwepo wako

Bali unaweza kuondoka taratibu, kimya kimya na kwa utulivu mkubwa sana pasi na ulazima wa kuacha alama mbaya kwake (kwao).

Hakuna tuzo ya kelele bali zipo tuzo za heshima na utii,

Ukiondoka bila kelele itakujengea heshima kubwa sana hata kwa huyo unaejitenga nae na bila kusahau wanao kuzunguka kwa ujumla.

Kaa kimya na ondoka nenda kaanze upya utapata mtu anae stahili thamani yako,

Mtu (watu) watakao kulipa thamani sawa na ile unayotoa bila kutumia nguvu kubwa sana

Kumbuka maisha hayana tuzo za kelele.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Uzito Wa Hoja Hupimwa Kwa Hoja Nzito Zaidi Kwa Maana Hakuna Mzani Wa Hoja

Next Post

Kabla Hujachukia Jiko La Mafiga, Hakiki Ubora Wa Kuni Unazotumia Kwanza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.