
Huo Mbuyu mkubwa sana, unaokutisha kila ukipita chini yake kwa ukubwa, urefu na Uimara wake kuanzia mizizi, shina mpaka matawi
Kumbuka nao pia ulianza kama mbegu ndogo ya mchicha!
Ukakuwa taratibu kwa kujenga himaya yake chini kwa chini kwanza
Mbuyu ulianza kutengeneza mizizi imara ndani ya ardhi kabla ya kupanda kujenga himaya kubwa kwa juu ya ardhi,
Kama mbuyu usingejenga mizizi imara na migumu pia isingiwezekana kuwa mkubwa sana kwa juu
Hakuna anaejua mangapi yalifanyika ndani ya ardhi kabla ya kuonekana mkubwa sana kwa juu mbele ya macho ya kila anae utazama!
Hivyo Basi usiogope kuanzia chini, usikate tamaa kutengeneza himaya yako, usijione mnyonge kwa kuanza na kidogo
Kumbuka wakati unaanzia chini ndio wakati unatengeneza himaya yako na misingi imara kwa ndani kabla hujaweka himaya kwa nje.