Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Hata Sukari Ni Tamu Ila Ikizidi Sana Hukera, Fanya Mambo Kwa Kiasi

Ukionesha sana mapenzi yaliyo pitiliza kwa mtu, atakuchoka na kukuona boya na ukipunguza zaidi utamkosa!

Ukionesha sana wema kwa watu, watakuzoea na kukuona sehemu ya kukupiga mizinga au hata hujielewi na huna malengo, na ukiacha kabisa watasema una roho mbaya!

Ukitangaza sana bidhaa au huduma yako kiasi cha kupitiliza au hata kutoacha nafasi ya watu kutafakari, wataichoka na kuidharau! na ukiacha kabisa watasahau

Ukiomba omba sana utachokwa na kushusha thamani yako na ukiacha kuomba omba kabisa hutopewa!

Ukiwa mcheshi sana kupitiliza ni tatizo na ukinuna sana ni tatizo zaidi

Ukitumia nguvu nyingi sana kwenye kutafuta maisha ni tatizo na ukiwa mvivu ni tatizo zaidi!

Hata ibada haifanywi kila wakati na kupitiliza maana ikizidi sana (mifano ipo mitaani kwetu) na hata,

Mungu amesema Asiye fanya kazi na asile kwa maana huwezi kuweka ibada kama sababu ya kuacha maisha mengine!

Na ukiacha kabisa Ibada ni mtihani mkubwa zaidi!

Kitu cha kuzingatia ni….

Fanya mambo kwa kiasi na kipimo maalumu ili kuepuka kupoteza ladha na maana au hata lengo ulilonalo!

Hata sukari huhitajika kunogesha ladha ya utamu na inapendwa na kila mtu Ila ikizidi ni mtihani mkubwa sana na hupoteza ladha nzima

Chukulia mfano wa chai au chakula chochote kinachohitaji sukari kisha zidisha kiwango cha sukari au usiweke sukari kabisa (utapata majibu sahihi)

Hivyo anza kuweka kipimo sahihi cha mambo hata vijana husema (jifunze ku balance shobo)

Usiwe mwepesi sana wala mgumu sana kupindukia

Usiwe mrahisi sana wala mzito sana

Usijipendekeze sana wala kujisikia sana

Pima kipimo sahihi kwa wakati sahihi ili uweze kufurahia maisha yako!

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Kama Huwezi Kuchagua, Kubali Kula Wa Chuya

Next Post

Uliza Ujue Ukweli, Sio Kila Jambo Lipo Kama Unavyoliona Au Kulisikia Kwa Wengine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.