
Huhitaji kujua kila kitu ili kuanza kufanya kitu na kufanikiwa
Huhitaji kuwa na kila kitu ili kuanza kufanya kitu na kufanikiwa
Huhitaji kuwa na sapoti kutoka kwa mtu mwingine ili kuanza kufanya kitu na kufanikiwa
Wala huhitaji wengine kukushangilia na kukuambia unaweza ili kubusti hamasa yako.
Bali unahitaji utayari wako binafsi kutoka ndani yako wewe mwenyewe kwanza
Unahitaji sapoti yako wewe na wewe mwenyewe binafsi kwanza
Unahitaji nia na dhamira ya dhati kutoka ndani yako wewe mwenyewe kwanza.
Kwenye maisha wengine huja baada ya kuona umefika mahala fulani,
Lakini pia vingine huja baada ya kuona umeweza kutumia ulivyo navyo kwanza.
Maisha hayataki maandalizi makubwa sana kuanza Ila yanahitaji nidhamu ili kuendelea,
Maisha hayataki ukamilifu ili kuwa bora bali yanataka kuanza na kurekebisha makosa ukiwa safarini
Maisha na mafanikio yanataka kuona hatua yako ya kwanza wewe binafsi kabla hayajavutana na kukusogelea!
Kutumia muda mwingi kuwaza sana sio silaha ya kukupa kile unataka, bali hatua ya kwanza utakayo chukua inaweza kuleta mabadiliko milele!
Acha kuwaza sana badala yake geuza mawazo yako kwenye utendaji wa vitendo kwanza.
Kuna uwezekano mkubwa mawazo uliyonayo miaka yote kama ungeweka kwenye vitendo basi ungekuwa mbali sana.
Usiendelee kungoja hamasa jilazimishe na jihamasishe wewe binafsi kwanza hapo hapo ulipo kwa kutumia hiko hiko kidogo ulichonacho.
Unaweza ukiamua, Anza sasa.