
Kuna ile Roho ambayo hukukataza kila jambo lako zuri unalotaka kufanya
Roho ya kushindwa hukutawala kila unapotaka kujikomboa
Roho ya kuona mabaya kwenye kila zuri lilipo mbele yako
Roho inayokuvuta nyuma kila unapotaka kusogea mbele
Roho inayo sema hapana hata pale palipo andikwa ndio
Roho inayokwambia huwezi na huna thamani kama wengine
Roho inayokutawala ili ujione mnyonge sana mbele za wengine
Roho inayo ondoa hamasa ya kufanya chochote kizuri unachotaka kufanya .
Hii ndio wengi huita Roho ya umasikini na wengi zaidi huamini kuwa wamerogwa!
Ukweli ni kuwa Roho hii ipo ndani yako wewe mwenyewe na wewe ndio uliye Ipandikiza!
Umeipandikiza kwa kuipa nguvu (kuiabudu kwa kila inachotaka)
Kwa maana kila inapokushawishi na wewe hukubali.
Siku ambayo utaamua kuitoa kabisa kwenye maisha yako, elewa kuwa unazo nguvu na uwezo huo wewe mwenyewe
Huhitaji maombi ya kukemea wala Mganga wakuagua
Unajihitaji wewe mwenyewe, wewe ndio mwenye himaya wa hio Roho na wewe pekee unayo dawa ya kuondoa hio Roho.
Dawa kubwa zaidi uliyonayo ni nia na Imani
Amua tu kuwa kuanzia sasa siitaki hii Roho kabisa kwenye maisha yangu
Kuanzia muda huu naanza upya na kamwe sito ruhusu Roho hii itawale kwenye maisha ninayoishi
Mimi ni mshindi hata kabla ya kukumbwa na Roho hii na bado nitakuwa mshindi hata baada ya kuondoka kwa Roho hii.
Sema kwa nguvu zako zote kuwa kwa sasa sitoruhu kutawaliwa tena na Roho yoyote
Chukia kwa dhati kabisa kutoka moyoni hasara ambazo hio Roho imekusababishia.
Halafu anza kufanya kila kinacho kutisha sana au kukuogopesha zaidi
Fanya kwa ujasiri na kamwe usiache mpaka uridhike kabisa kwa matunda utakayoona.
Kila utakapo hisi roho ile inakukataza au kukusema kitu chochote kibaya basi ikatae kwa kufanya kile inachokukataza kwa nguvu zaidi na zaidi
Mfano Roho ikikutaka uache kazi unayofanya, na kwenda kulala (maana yake hio ni roho ya uvivu) sasa jiambie kamwe siendi kulala mpaka nimalize hii kazi na siipi hii roho ushindi,
Au kila unapotaka kuanza kitu na ukahisi Roho inakupa sababu za kutoanza (hio ni Roho ya umasikini) Jiambie naanza sasa kufanya na kamwe siipi hii Roho ushindi maana ikishinda basi na mimi nimekubali kuwa masikini milele.
Fanya hivyo, nenda kinyume kwa kila roho inayokuvuta nyuma na kamwe usikubali kuipa Roho yoyote ushindi.