
Hujaumbwa kuteseka, mateso unataka wewe mwenyewe
Maisha ni mepesi mno na rahisi kwa kila mmoja wetu kwa namna ambavyo muhusika huchagua
Kama kawaida Mungu Hakuumba watu wake waje kuteseka kwenye Dunia yake
Mateso na maumivu husabisha mtu binafsi kulingana na machaguo anayotaka
Ukiona unaishi aina fulani ya maisha, yawe mazuri au mabaya elewa kuwa wewe ndio mchaguzi
Ukiona maisha yako ni magumu sana au hata yanayo boa na kuchosha, Elewa kuwa wewe ndio chanzo
Maisha ni rahisi na mepesi sana kama utaamua kuchagua upande wa urahisi
Maisha ni matamu sana kama utaamua kuchagua upande wa kuona utamu wake.
Elewa kuwa namna unavyoona watu wabaya ni kwakuwa umechagua kupenda watu wasio kupenda wala kukuhitaji,
Unaona maisha magumu sana kwakuwa unataka vitu nje ya uwezo wa kipato chako halisi!
Unaona maisha machungu kwakuwa haupo katika mazingira sahihi unayopaswa kuwa
Unaona maisha mabaya hayana ladha kwakuwa umechagua kuona mambo mabaya badala ya mazuri
“Badili namna unavyo fikiria na kuchukulia mambo, zungukwa na wale wanaokupenda kisha rahisisha mahitaji yako ya kila siku na utapata tafsiri sahihi ya maisha yako”
Kila mmoja anapaswa kuishi maisha yake kwa njia zake sahihi ili aweze kuyafurahia maisha
Kamwe huwezi kuishi maisha ya mtu mwingine halafu utegemee furaha ya maisha
Huwezi ishi kwa kutaka vitu nje ya uwezo wako kisha utegemee furaha
Nunua vitu vilivyo ndani ya uwezo wako na vitu muhimu zaidi kwa wakati huo,
Kula bata kwa kiwango cha kipato chako na maeneo rahisi zaidi
Vaa nguo za kipato chako sio kutaka kuonekana unazo kumbe huna
Usiwaze macho ya watu pengine hata wao kuna muda wanataka kuwa kama wewe
Kila mmoja ana siri nzito kuhusu maisha anayo ishi!
Hivyo kamwe hupaswi kutamani maisha ya mtu mwingine.
Huwezi kujilinganisha na wengine waliokuzudi kisha utegemee furaha
Hakika Dunia sio sehemu ya bahati mbaya kwa mtu yoyote
Hujaumbwa Kwa bahati mbaya wala Mungu hakukosea kukuumba.
Unajipa mawazo na maumivu yasiyo na msingi wowote
Ishi ndani ya njia zako kwa maana halisi ya maisha yako
Yape maisha tafsiri sahihi iliyo ndani ya uwezo wako
Kisha pambana kutanua maana au tafsiri ya maisha yako taratibu
Usijipe presha wala haraka kutaka vitu ambavyo bado huna uwezo navyo kwasababu utaishia kupata maumivu moyoni .