
Kuna kanuni ndogo ndogo sana za maisha ambazo hufanya watu wengi wateseke bila kujua
Haijalishi una mbio kiasi gani, vipepeo havikimbizwi!
Hata kama una uwezo wa kupaa na kufika umbali kama wao,
Bado huwezi kamata idadi kubwa ya vipepeo kwa njia hio!
Unaweza kukamata idadi chache sana na wakati huo huo ukawa hoi kwa uchovu!
Njia nzuri zaidi kama kweli unataka vipepeo wengi iwe kwa mara moja au milele
Ni
“Kujenga bustani nzuri yenye kuvutia, iliyo sheheni maua mbali mbali na harufu nzuri zaidi “
Ukiwa na bustani nzuri basi huwezi pata shida kabisa kutafuta Vipepeo unaotaka
Kwani watakuja, watajaa, wataitana, watazaliana na kuweka makazi ya kudumu hapo!
Kwenye maisha yako kama unataka vitu vingi bila kutumia nguvu basi tengeneza mazingira sahihi vije kwako
Mazingira ambayo huvutia hivyo vitu bila kuumiza kichwa sana wala kutumia nguvu kubwa kila wakati
Mazingira huambatana na mipango au mikakati sahihi kwa wakati sahihi
Mfano kama unataka wateja wengi, usilazimishe wateja kuja kwa nguvu utachoka! Badala yake wape thamani wanayotafuta na watakuja wao wenyewe!
Unataka pesa: Usikimbizane na pesa kwa nguvu kwasababu utachoka bure, badala yake weka mifereji sahihi kisha pesa zitiririke kwako bila shida na ziwe za kudumu sio mara moja!
Unataka watu wakupende, usiwalazimishe sana kwa ushawishi wa nguvu na maneno matupu bali wape thamani yako waione na kuihisi kwenye mioyo yao kisha wataongozana kwako wao wenyewe!
Unataka furaha na amani, usiitafute mahala popote kwa nguvu, bali tengeneza mazingira mazuri ya utulivu kuanzia ndani na nje yako kisha utapata amani na furaha bila shida.
Hivyo hivyo kwa kitu kingine chochote kile, usikimbizane nacho kamwe utaumia bure
Elewa udhaifu wa hiko kitu, kisha kitege kwa mtego sahihi
Tengeneza mazingira mazuri, yenye kuvutia kitu hiko kinase chenyewe mtegoni kwako!
Maisha hayataki nguvu kubwa, maisha ni mipango na mikakati
Wengi wanachukia Dunia, wakati Dunia ipo kwa ajili ya kuwapa kila wanachotaka!
Chunga usiwe mmoja wao!