
Watu wengi mno wanateseka kwenye maisha kwa mambo madogo madogo sana
Mambo ambayo yako ndani ya uwezo wao wenyewe na wanalimudu bila shida
Neno HAPANA ni dogo mno Ila limeharibu malengo na ndoto za watu wengi mno Duniani
Ile hali ya kuwa maharage ya mbeya hata kwenye vitu visivyotaka urahisi wako
Kuna vitu sema hapana haijalishi ni kwa mtu, watu au kitu
Usiogope matokeo yatakavyokuwa baada ya kukataa
Ikiwa kitu hakipo ndani ya uwezo wako, wala hakina faida na wewe sema HAPANA
Endapo jambo linaenda kuvuruga bajeti zako na mfuko wako sema HAPANA
Endapo kitu kinaenda haribu akili yako na hata kukupa msongo wa mawazo kikatae kwa nguvu
Ikiwa unaona ratiba zako zitavurugika na kukutoa nje ya mipango kataa kwa nguvu kubwa
Usiogope kuchukiwa wala kusemwa vibaya kamwe kisa kusema hapana
Binaadamu hawaridhiki hata uwape nini, watakusema tu
Mtu akiamua kuona mazuri yako atayaona tu hata kati kati ya mabaya uliyonayo
Na mtu akiamua kuona mabaya yako haijalishi uwe mwema kiasi gani atakuchukia tu
Ipe nafsi yako uhuru na amani kwa kuongeza uwezo wa kusema HAPANA
Jizingatie kwanza wewe kabla ya wengine
Furahia muda wako kabla ya kuugawa kwa wengine
Furahia pesa zako kabla ya kuzigawa kwa wengine
Acha wakuchukie, acha wakuone mbaya, acha wakusema vibaya hilo sio jukumu lako
Zingatia amani ya nafsi yako, zingatia maisha yako, zingatia muda na kipato chako
Ishi maisha unayoona yanafaa bila kuzingatia watu au vitu vingine utaumia bure
Siku utayo weza kusimama na kusema hapana bila hofu wala uoga, Ndio siku utakayo anza kuishi Rasmi
Hakuna raha kwenye maisha kama uwezo wa kukataa bila kuogopa mtu au mazingira.