
Kadiri unavyo shukuru Ndivyo unavyojisogeza karibu na mafanikio yako
Jifunze kuwa na moyo wa kuyaona mazuri badala ya mabaya
Punguza kulalamika kila mara kwenye mambo hasa madogo madogo
Moyo wa shukran ni moyo uliojaa amani na baraka
Ukiwa unashukuru mara kwa mara itakusaidia kufungua Dunia yako chanya
Dunia yenye kuona mazuri na kuchukulia kila jambo kama fursa na mwanzo mpya wa maisha mengine
Epuka makasiriko, malalamiko, na kujilinganisha kwa wengine
Ishi katika njia zako, tafuta maisha yako na shukuru kwa kila hatua unayopiga.