
Kabla hujataka kupewa hebu anza kutoa wewe
Kabla hujataka kusaidiwa Jaribu kwanza kutoa msaada wewe
Kabla hujataka kuonewa huruma, jifunze kuonea huruma wengine
Kabla hujataka kushirikishwa, anza kushirikisha wengine
Kila mmoja ana uhitaji eneo fulani na hakuna aliye kamili ka hata kama ana mafanikio makubwa
Usipende sana kujiona kama muhanga wa mambo kuliko wengine
Hakuna mtu aliyeletwa kusaidia wengine bila yeye kupokea msaada
Kabla hujaanza kulaumu wengine kuwa hawakusaidii hebu jiulize wewe umewahi kuwasaidia nini?
Kabla hujasambaza ubaya na chuki kisa kunyimwa au kukataliwa, jiulize una mchango gani kwa huyo aliyekukatalia?
Badala ya kujenga uhasama na chuki anza kuonesha umuhimu wa wewe kupewa!
Wape wengine kwanza kisha subiri kupokea!
Usipende sana kujiona kama una mapungufu kuliko wengine!
Watu wana mapungufu zaidi yako Ila wanajikaza kwa sababu wanajua kuwa maisha yao ni jukumu lao
Hatuwezi kujenga furaha, amani na maendeleo kwa kupenda kuombana ombana hata kwa vitu visivyohitaji msaada!
Kila mmoja ana paswa kusimamia maisha yake binafsi kwanza, kusaidia wengine kwanza kabla ya kusaidiwa au kupokea msaada
Misaada Ndio chanzo kikubwa cha uvivu wa kufikiri na kutenda kwenye maisha ya watu wengi
Acha watu wafurahie mafanikio ya jasho lao pasi na kubebeshwa lawama zisizo na msingi
Beba majukumu yako, simamia hatima yako
Unaruhusiwa kuomba Ila hupaswi kujenga chuki baada ya kunyimwa.