
Kabla ya kukimbilia kutaka mafanikio au faida onesha uwezo
Kabla ya kutaka kujulikana na kupewa nafasi, onesha uwezo
Kabla ya kutamani kupewa kipaombele, onesha uwezo
Kabla ya kupewa kazi na tenda unazotaka, onesha uwezo wako
Kabla hujasema huna bahati na kuhisi umerogwa, hebu onesha uwezo kwanza
Kabla hujatangaza kuwa kuna watu wana pendelewa kuliko wewe, waoneshe uwezo kwanza
Hakuna namna yoyote ya kuaminika kama hujatoa sababu za kuaminiwa!
Dunia ina watu wengi sana wenye uwezo wa aina mbali mbali kwahio sio rahisi wewe ufungie uwezo wako ndani kisha utarajie kutafutwa kwa tochi!
Kila mtu yuko bize na mambo yanayo onekana kwa macho mbele yake!
Hakuna ambae atapoteza muda wake kutafuta ubora wako ambao haupo kwenye macho yake..
Simama kwanza jiamini, onesha uwezo wako kwao kisha watakupa nafasi unayotaka.
Hata kama una uwezo mkubwa na ubora sana kwenye jambo fulani, kama hauto onesha kwa vitendo elewa kuwa hakuna atakae jua kamwe
Kuna muda utapaswa kujitolea bila malipo kabisa..
Kuna muda utapaswa kupokea malipo kidogo
Na kuna muda utapaswa kufanya na kuanza na ulichonacho kwanza kwa ugumu huo huo
Lengo kubwa ni KUONEKANA!
Wape sababu za kukuchagua na kuacha wengine kwa vitendo
Wape sababu za kuona umuhimu wako na faida yako
Kisha watawaacha wengine na kukupa wewe unachotaka…..
Jitokeze, wakuone, wakujue, wakuamini kisha wakuchague.