Life With Muhasu » You Can Win If You Want

Kama Huwezi Kuchagua, Kubali Kula Wa Chuya

Wakati nalelewa kwa babu yangu kigoma, bibi alikuwa mwalimu wangu mkubwa kwenye kazi za nyumbani kwetu

Alinifundisha kufanya kazi zote japo kwa ukali sana ila mpaka sasa amekuwa msaada mkubwa kwenye maisha yangu ya sasa kupitia mafunzo yake ya zamani,

Bibi alipenda sana kutumia neno la “utakula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua” mara kwa mara

Hasa pale nilipo onesha hali ya kuchoka na kutaka kuripua kazi ili ziishe nipumzike haraka.

Sikuwa naelewa sana kwa undani maana ya kauli ile, nilichukulia maana ya kawaida sana kutokana na umri wangu mdogo.

Baada ya kuwa mkubwa na kuingia kwenye maisha ya kutafuta ndio nikaweza kuelewa zaidi maana ya kauli ya Bibi.

Kula wa chuya (mchele ambao umechanganyika na maganda ya mpunga yaliyo kobolewa)

Maana yake ni kuwa , mchele huo baada ya kupikwa utakuwa na ladha ya wali, Ila wali ambao hauna ladha kamili wala raha kamili ya wali.

(vuta picha unapokulaga wali uliojaa chuya utaelewa zaidi)

Kero ya maganda ya mpunga (chuya) kwenye wali hupunguza ladha kamili ya wali ambayo mlaji alipaswa kuipata

Hivyo mlaji hupata ladha ya wali kwa sababu anakula wali Ila hapati ladha ya wali ambayo ndio haswa hupaswa kusikika kwenye wali kwa sababu tu ya uvivu wa kuchagua chuya.

Tuna zungukwa na marafiki ambao tunahisi ni marafiki sahihi kwa sababu wanatuonesha matendo ya kirafiki!

Lakini hatupati matendo zaidi ambayo humaanisha urafiki wa dhati kwa sababu ya uvivu wa kuchagua marafiki sahihi!

Tunaishi na wapenzi ambao hutuonesha vitendo vya kimapenzi kisha tunaridhika na kuhisi tunapendwa,

Wakati sio vitendo kamili tulivyopaswa kupewa na wapenzi sahihi kwasababu ya uvivu wa kuchagua wapenzi sahihi!

Tunaridhika na maisha tunayo ishi kwa sababu tunaona kama tunaishi vizuri, Ila hatuishi ndani ya maana na kusudi sahihi la kuumbwa kwetu na kufurahia maisha kwa kiwango tulichopaswa kufurahia kwa sababu ya uvivu wa kutafuta kusudi la maisha sahihi!

Tunaridhika na viongozi wanao tuongoza, kwa sababu wanatuonesha vitendo vya uongozi, Ila hatupati faida kamili ya uongozi kwa viongozi wetu kwa sababu ya uvivu wa kuchagua viongozi sahihi.

Kwenye maisha ukiwa mvivu wa kutoa chuya zako basi utaishia kupata kivuli badala ya picha halisi!

Najua ni ngumu kiasi kuelewa, Ila point ya msingi ni unapaswa kuchagua mambo sahihi zaidi ili uweze kufurahia maisha kwa usahihi zaidi

Ukiona mambo hayaendi vile unataka elewa kuwa hayo mambo yamechanganywa na chuya,

Hivyo ni jukumu lako kutenganisha kati ya chuya na mchele ili upate wali mtamu.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Tumia Mshahara Na Kipato Chako Binafsi Kusapoti Biashara Yako Mpaka Pale Biashara Yako Itakapoweza Kusapoti Kipato Na Maisha Yako

Next Post

Hata Sukari Ni Tamu Ila Ikizidi Sana Hukera, Fanya Mambo Kwa Kiasi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy makala hii.